Na HEMEDI MUNGA, Iramba
KUTEGEMEANA kwa wananchi na mazingira yanayowazunguka wanadamu hususan misitu imeelezwa kuwa biashara kubwa kufuatia mbadiliko yanayoendelea kutokea duniani.
Aidha, wametakiwa kufahamu kuwa mabadiliko yanayoendelea kutokea duniani licha ya kuwa na changamoto hasi ispokua yamekua kua na mambo chanya ambayo yamegeuka kuwa fursa za kibiashara kuhusu hewa ya ukaa.
Akizungumza na wananchi wa kata ya Ndulungu wilayani Iramba mkoani Singida, Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi na Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amesema dunia imekua ikibadilika kwa sababu kipindi cha nyuma watu walikua wanapata fedha kwa kuchoma mkaa.
Amesema hivi sasa kuna baadhi ya vijiji ambavyo vinadaiwa kuwepo nchini ikiwemo wilayani Tanganyika kuna watu waliotunza Misitu wanauza hewa ya ukaa inayotengenezwa kutokana na misitu.
Ameweka wazi kuwa waliuza nishati hiyo wakapata takribani sh bilioni nane ambazo zinawasaidia kujenga ofisi za kisasa, wanatengeneza madaraja ikiwemo mabweni.
"Ndugu zangu katika msitu huo, kinachovunwa hakionekani ni hewa tu, ukiwa na msitu umeshonana, wataalamu hao wanaupima na kutegesha mitambo yao huku wakivuna hewa ya ukaa ambayo wanaiuza," amesema Dk. Nchemba na kuongeza kuwa:
Sasa hiyo ni rahisi maana unatunza msitu halafu unauza hewa kitu ambacho hakimtoi mtu jasho ukilinganisha na kuchoma mkaa."
Kutokana na hali hiyo, Dk. Nchemba amesisitiza kuwa dunia imebadilika, hivyo eneo lolote linaloweza kuwa ni pori walitunze kweli kwa sababu ni hela hizo hivi sasa.
Aidha, amefafanua kuwa teknolojia hiyo inasaidia wananchi kuvuna fedha, hivyo inakua ni msaada wa kutatua changamoto ndogo ndogo kuanzia ngazi ya kijiji au kitongoji.
Ameongeza kuwa kufuatia dunia hiyo kuwa na mabadiliko haya, ikiwa wĂ navuna namna hiyo kila mwaka, hivyo waende wakatuze misitu kwa sababu sasa hivi misitu ni biashara.
Pia, ameeleza kuwa biashara hiyo haitaji kuwa ni misitu ya kupanda au kumwagilia inaweza kuwa miti ya kawaida tu iliyotengeneza kapori, hakika itawasaidia kuuza hewa ya ukaa na kununua majiko ya gesi.
Akizungumza kwa nyakati tofauti, Mkuu wa wilaya hiyo, Suleiman Mwenda ameendelea kumshukuru na kumpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuijali wilaya hiyo kwa sababu aliipatia fedha nyingi.
DC Mwenda amesema rais huyo amehakikisha kila kata ndani ya wilaya hiyo yenye kata 20 ikipewa takribani sh bilioni 2.4 ambazo zimekua zikijenga na kutengeneza miradi ya maendeleo ambayo imetajwa kuwa mwarobaini wa changamoto zinazodaiwa kuwakabili wananchi katika sekta zote.
"Ndugu zangu niwaombe tuendelee kumuunga mkono Rais wetu, hakika ametujali mno, haijawahi tokea tangu wilaya hii kuwa, shukran sana Rais wetu," amesisitiza.
Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba akiwataka wananchi kukimbilia fursa itokanayo na utunzaji wa misitu kwa kuuza hewa ya ukaa, leo wakati akiongea na wananchi wa kata ya Kata ya Ndulungu wilayani Iramba mkoani Singida. (Picha na Hemedi Munga)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇