LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 16, 2024

MADAWATI YA JINSIA NA WATOTO 420 YAMEANZISHWA JESHI LA POLISI





Na John Banda, Dodoma

JESHI la Polisi nchini  limeanzisha madawati ya Jinsia na Watoto 420 ili kukabiliana na  matukio ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto katika jamii.

Hayo yamebainishwa jijini hapa leo Aprili 15,2024 na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini Hamad Masaun wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya wizara hiyo katika kipindi cha miaka 60 ya muungano.

Amesema kutokana na kuongezeka kwa matukio ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto, serikali ilianzisha dawati maalumu la kushughulikia matukio hayo ili kuwalinda watoto kuishi katika mazingira salama na hatimaye kutimiza ndoto zao.

“Uanzishwaji wa madawati ya Jinsia na watoto umesaidia kuandaa askari wenye mafunzo maalum ya kutoa elimu juu ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya Watoto kwa makundi yote katika jamii.

Ameongeza kuwa Kupitia Madawati hayo huduma bora ya namna ya kuwahudumia waathirika wa vitendo vya ukatili wa kijinsia imewezeshwa.

Aidha Waziri Masauni amewaonya wanaotumia Mitandao ya kijamii kuwakashfu na kuwatuna Viongozi wa serikali Pamoja na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba Sheria zipo na hazijalala.

“wanaotukana na kuwakashfu viongozi kupitia mitandao ya kijamii Serikali inawafuatilia na hakuna atakayepona hata kama kwa sasa bado hajakamatwa lakini anafuatiliwa, wale ambao wanayasapoti matusi na kashfa hizo mitandaoni waangalie isije ikawa wao ndio rahisi kupatika”, amesema na kuongeza





 

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages