LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 15, 2024

UCHAGUZI MKUU SENETI VYUO NA VYUO VIKUU KESHO MACHI 16. KAWAIDA AWAFUNDA UVCCM

Na Mwandishi Maalum, Ihemi,ringa
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mohamed Kawaida, amesema Jumuiya hiyo imeanza utekelezaji wa kufuatilia fedha za asilimia 30 zilizotolewa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kutekeleza miradi kwenye Halmashauri zote.

Kawaida ameyasema hayo wakati akifungua  mdahalo wa Seneti ya vyuo na vyuo vikuu  katika ukumbi wa Chuo Cha Ufundi cha Ihemi mkoani Iringa.

Mdahalo huo, umehusisha vyuo na vyuo vikuu nchini ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mkuu wa viongozi wa Seneti wa vyuo na vyuo vikuu unaotarajiwa kufanyika  kesho Machi 16.

Kawaida,aliwataka vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa na serikali ikiwemo mikopo ambayo hutolewa na Kila Halmashauri.

Amesema UVCCM  itahakikisha fedha fedha hizo ambazo hutolewa na Rais asilimia 70 kwa kila Halmashauri Nchini zinawafikia walengwa na kufanya kazi iliyokusudiwa.

MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mohamed Kawaida, akifungua  mdahalo wa Seneti ya vyuo na vyuo vikuu katika ukumbi wa Chuo Cha Ufundi cha Ihemi mkoani Iringa, leo.



 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages