Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Prof. Joseph Ndunguru,akiwasilisha utendajii na mafanikio ya TPHPA kwa mwaka 2023/2024, katika kikao kazi baina yake na Wahariri wa Habari, kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kufanyika Jijini Dar es Salaam, Machi 13, 2024.
---------------------------------------
Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
MAMLAKA ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), imesema ipo imara kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kupitia Msajili wa Hazina la kufanya mageuzi katika Taasisi zake za Serikali (Reform, Rebuild, Resilience and Reconciliation (4Rs) ili kuleta tija.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Prof. Joseph Ndunguru, akiwasilisha utendajii na mafanikio ya TPHPA kwa mwaka 2023/2024, katika kikao kazi baina yake na Wahariri wa Habari, kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kufanyika Jijini Dar es Salaam, Machi 13, 2024.
Amesema Ili kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo kama Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia, mambo muhimu ambayo TPHPA inayazingatia ni pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi lakini pia kuwekeza kwenye utafiti, jambo ambalo serikali imefanya kwa kiasi kikubwa
“Kama mjuavyo bajeti ya kilimo imefikia sh. bilioni 970.78 na nguvu kubwa imeelekezwa kwenye Utafiti wa mbegu bora, Uzalishaji wa mbegu na miche bora, usambazaji wa mbegu na miche ya ruzuku, kuwekezaji kwenye huduma za ugani na ujenzi wa miundombinu ya kilimo, vyote hivi ni kufanya kilimo kinachotumia sayansi na teknolojia na hivi vinaenda kuleta faida kubwa katika kilimo.” akasema Prof. Ndunguru.
Kuhusu mafanikio, Prof. Ndunguru alisema Mamlaka ya TPHPA imevunja rekodi ya Mapato ya Ndani, baada ya kukusanya kiasi cha Sh. Bilioni 6.1 katika kipindi cha miezi mitatu tu kuanzia Juni hadi Septemba 2023, makusanyo ambayo ni sawa na asilimia 95.2 ya makadirio ya makusanyo ya mwaka mzima kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali vya mapato ya ndani (own resources).
Alisema katika mwaka wa fedha wa 2023/2024 Mamlaka iliweka lengo la kukusanya kiasi cha Sh. Bilioni 6.4, lakini ndani ya miezi hiyo mitatu hadi kufikia Septemba ikakusanya Bilioni. 6.1 na kubainisha kuwa matarajio ni kuvunja rekodi zaidi ifikapo mwisho wa mwaka huu.
“Ni wazi kwamba, hadi kufikia mwisho wa Mwaka wa Fedha, TPHPA itakusanya zaidi ya asilima 100 ya makadirio hayo na hivyo kuongeza kiasi cha gawio lake kwa Serikali Kuu ambalo linakuwa ni asilima 15 ya pato letu.
Hii maana yake ni nini? Kwa makadirio ya awali, tungeweza kutoa gawi la Serikali la Sh. Milioni 968, lakini kwa aina ya rekodi tuliyoweka ya makusanyo kwa Mwaka wa Fedha, maana yake gawio la Serikali Sasa litapanda na kufikia Sh. Bilioni 3.6," alisema Prof. Ndunguru.
Taarifa kamili aliyowasilisha Prof. Ndunguru hii👇






































































No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇