LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 16, 2024

MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI CCM AANZA ZIARA RASMI KAGERA


Na Lydia Lugakila, Biharamulo


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Fadhil Rajab Maganya kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ameanza rasmi ziara yake ya kikazi mkoani Kagera Marchi 15, 2024 katika wilaya ya Biharamulo.


Akiwa wilayani Biharamulo Mwenyekiti huyo alikagua kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na miradi inayotekelezwa na Chama na Jumuiya zake pamoja na miradi inayotekelezwa chini ya Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Katika ziara hiyo Fadhil aliambatana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera Nazir Karamagi sambamba na Wajumbe wa Kamati ya siasa ya Mkoa, na kamati ya Utekelezaji ya Wazazi Mkoa.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages