LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 8, 2024

MABORESHO YA RAIS DK. SAMIA SEKTA YA AFYA NDANI YA MIAKA MITATU YAUPAISHA ZAIDI MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF)

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bernard Konga, akizungumza alipokuwa akiwasilisha Mafanikio ya Mfuko huo katika miaka mitatu ya Rais wa Serikali ya Awamu ya Sita Dk. Samia suluhu Hassa, kwa Wahariri na Waandishi wa habari katika kikao kazi, kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa hazina na kufanyika jijini Dar es Salaam, Machi 7,2024. PICHA ZAIDI BOFYA 👉HAPA

------------------------------------------

Na Bashir Nkoromo, Official CC Blog
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umethibisha kwamba Maboresho yaliyofanywa na Serkali katika sekta ya Afya katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais wa Awamu ya Sita Dk. Samia Suluhu Hassan umewezesha Mfuko huo kupata mafanikio makubwa.

Umesema katika Awamu hiyo ya Rais Dk. Samia, Mfuko huo umeendelea kuboresha kitita chake na kutoa kitita cha mafao chenye wigo mpana ukilinganisha na skimu zingine za Bima ya afya.

Hayo amesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bernard Konga, katika kikao kazi baina yake na Wahariri na Waandishi wa habari, kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kufanyika Alhamisi Machi 7, 2024, Jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho Mkurugenzi Mkuu Konga, ameeleza mafanikio lukuki na kuanisha mipango ya baadaye ambayo NHIF itayatekeleza hadi kuingia miaka minne ya Uongozi wa Rais wa Awamu hiyo ya Sita Dk. Samia, Tafadhali isome taarifa hiyo, kama alivyoiwasilisha Mkurugenzi huyo.👇👇

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages