LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 18, 2024

MAONI YA MDAU WA SOKA BAADA YA STARS KUFUNGWA 3-0 , ASEMA TATIZO NI KARIA

Na Yahya Msangi, Mtanzania anayeishi Togo
Hatuwezi kupona kama hatutambui tatizo. Tatizo ni Karia. Mimi nilihoji ilipokuja Twiga Stars kucheza na Togo. Nilihoji na niliambiwa tatizo ni Mkiti TFF. Anaingilia mambo ya kiufundi. Anatawala kila kitu (over governance). Walipokuja Twiga Stars niliona haya na nikahoji:

1. Kuna mdada aliyeongozana na msafara ambaye bila hata DNA test utabaini ni ndugu wa damu na Karia. Photocopy ya Xerox machine! Ana madaraka makubwa mno. Ndiye aliyeenda kufanya manunuzi ya vyakula na masufuria Kwa bei ya kuruka. Mwanzoni niliombwa waje kupika nyumbani kwangu na nikawakubalia. Lakini huyu mdada na mwenzake mmoja wakaamua kununua masufuria kwa bei ambayo iliniacha nimeduwaa. Nikajua wamepiga cha juu. Ili kutimiza lengo lao wakaomba jiko la hotel wapike. Mkuu wa msafara akaniomba radhi sana Kwa usumbufu. Kama nasema uongo watu wachinguze ni kina nani walikuja na Twiga Stars Togo? Utamuonea huyu dada.

2. Timu haikuwa na nidhamu hata kidogo na ndio sababu ilishambuliwa kiwanjani. Pale hotelini baada ya kula tukijiandaa kwenda uwanjani niliingia kwenye lift na baadhi ya wachezaji. Walipanda wageni wengine. Wao wakawa wanawatukana wale wageni Kwa kiswahili. Wageni wale waligundua ni matusi japo lugha hawaielewi. Ulizuka mtafaruku uliofanya niwaombe wageni wale radhi kwa kifaransa. Nikawauliza wachezaji mbona hivi? Wakajibu kihuni tu. Matokeo tukayaona uwanjani. Nusura kocha auawe kwa chupa.

3. Timu ilipoingia kiwanjani wachezaji wote waliotoka nje wakapangwa. Nilikaa na baadhi ya wachezaji ambao siku Ile hawakucheza. Wao wanaishi Tanzania. Niliwadikia wakiwaita wale wa nje "wachezaji wa mwenyekiti"! Nikawauliza kulikoni? Wakaniambia hao wameletwa na Karia na wanapewa kipaumbele na upendeleo! Nikawatizama wanavyocheza. Ukolo mtupu. Kuna mmoja mrefu alicheza winga. Niliambiwa anaishi Sweden. Alikosa goli kipa keshatoka! Yeye na nyavu akampiga nje. Ilikuwa dakika 10 za kwanza za mchezo. Nikaamini wasemacho wale wadada. Nikakumbuka jinsi Hawa "maprofesheno" walivyokaa peke yao wakati tunakula hotelini!

Sikutaka kuyasema haya lakini mechi ya jana imenilazimisha niseme.

Tatizo ni KARIA. Na tusipotibu basi TAIFA NA TWIGA STARS Bora tuwahamishie Burundi.

Ni juzi tu kocha katuambia Kuna wachezaji mizigo! Karia akajibu hayo ni mawazo ya kocha sio ya TFF!

Kocha asingesema vile kama ndiye alichagua wachezaji! Hakika kocha kapewa wachezaji! Tusimlaumu. Jana kama sio uchawi tungepigwa kama kuleeeee kwa Mlandege! Uongo? 

Yahya Msangi

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages