LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 10, 2024

JESHI LA ZIMAMOTO LAANIKA TAARIFA YA UTENDAJI WAKE 2023, LAMSHUKURU RAIS DK. SAMIA KWA KUENDELEA KULIWEZESHA

Na Official CCM Blog
Jeshi linawajulisha kuwa katika kipindi cha mwaka 2023, lilikabiliana na matukio ya majanga ya moto, Ajali za barabarani, uokoaji nchi kavu na majini. Pia tumeendelea kufanya ukaguzi wa kinga na tahadhari dhidi ya majanga, kutoa elimu kwa umma pamoja na kufanya uchunguzi wa majanga mbalimbali.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limesema, katika kipindi cha mwaka jana (2023) watu 38 walifariki na148 kujeruhiwa katika matukio 2076 ya Moto, hali ambayo ikilinganishwa na mwaka juzi (2022) Idadi ya matukio, vifo na majeruhi iliongezeka.

Kwa mujibu wa Taarifa iloyotolewa na Jeshi hilo leo, idadi ya matukio kwa mwaka juzi (2022) yalikuwa 1,854 ambayo yalisababisha vifo vya watu 32 na Majeruhi 66.

Taarifa hiyo imeeleza  katika majanga mengine yakiwemo ya migodini, Jeshi hilo lilitoa huduma za Uokoaji katika matukio 1,195, ambayo yalisababisha vifo 684  na majeruhi 1,465, ikilinganishwa na matukio ya Uokoaji 567, vifo na Majeruhi 1,010 Mwaka uliopita 2022.

"Jumla ya maeneo 12,382 yalipatiwa elimu moja kwa moja na Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ikilinganishwa na maeneo 7,511 yaliyofikiwa mwaka 2022, Kupitia Vyombo vya Habari tumefanya jumla ya vipindi 728, ambavyo 606 ni vya Redio na 122 vya Luninga, ikilinganishwa na vipindi 602 vilivyofanyika mwaka 2022 ikiwa Redio 467 na Luninga 135", ilieleza taarifa hiyo.

Jeshi hilo lilizema. katika ukaguzi wa kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto tulifanikiwa kuyafikia maeneo 61,424 ambayo yalifanyiwa ukaguzi ikilinganishwa na maeneo 42,858 mwaka 2022, michoro ya ramani za majengo 2,431 zilipitishwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na kupata ushauri wa kitaalam ukilinganisha na michoro ya ramani za majengo 297 mwaka uliopita 2022.

"Tunauhakikishia umma tutaendelea kufanya ukaguzi wa kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto, kutoa elimu kwa umma, kushirikiana na Halmashauri za Miji na Majiji ili kuhakikisha tunapanga Miji yetu ili iwe salama wakati wa Majanga na kuliwezesha Jeshi kutoa huduma kwa wananchi kwa wakati bila kuwa na vikwazo vyovyote.

Tunatoa rai kwa Wananchi wote kutoa taarifa mapema wanapoona viashiria au tukio la Moto au ajali ya barabarani ikiwa kuna uhitaji wa huduma ya Uokoaji, wasisite kupiga namba yetu ya dharura ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji 114 ambayo ni bure kabisa.

Aidha, Tunapenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kuliongezea nguvu kazi, kupandisha vyeo vya Maafisa na Askari na kuliwezesha  fedha za miradi ya maendeleo ili kuongeza na kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma zake kwa Wananchi", lilieleza Jeshi hilo.



 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages