Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (Petroleum Bulk Procurement Agency - PBPA) Erasto Mulokozi, akitoa walisho lake, kwenye kikao kazi baina ya Wakala na Wahariri wa Habari, kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) na kufanyika jijini Dar es Salaam, leo Disemba 11, 2023. Picha zaidi Gonga👉 Hapa
Na Bashir Nkoromo, Official CCM Blog, Dar es Salaam
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za makusudi kupunguza makali ya bei ya mafuta nchini ikiwemo kutoa ruzuku kwenye gharama ya mafuta bei za nishati hiyo zinapopaa kutokana na changamoto mbalimbali za kidunia.
Katika ufanya hivyo, kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Julai 2022 hadi Disemba 2022 Serikali ruzuku ili kupunguza bei ya mafuta kwa wananchi iwe stahimilivu, hatua ambayo ilifanyika baada ya athari ya bei ya mafuta kupanda sana katika soko la dunia kutokana na vita baina ya Urusi na Ukraine.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (Petroleum Bulk Procurement Agency - PBPA) Erasto Mulokozi, kwenye kikao kazi baina ya Wakala na Wahariri wa Habari, kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) na kufanyika jijini Dar es Salaam, leo Disemba 11, 2023
Mulokozi alizitaja hatua nyingne zilizochukuliwa na Serikali kuwa kupitia Mamlaka zake imekuwa ikifanya ukaguzi wa mara kwa mara katika maghala ya kuhifadhia mafuta ili kuhakikisha taratibu za uendeshaji wa maghala hayo zinazingatiwa.
Pamoja na kueleza mengi kuhusu Serikali ya Awamu ya Sita kuhakikisha nishati ya mafuta inapatikana kwa wakati ikiwa bora na bei stahmilivu, Mulokozi alieleza pia malengo na mafanikio yaliyofanywa na yanayoendelea kufanywa na PBPA. Kuyajua kwa kina tafadhali soma taarifa kamili aliyowasilisha kwenye Kikao Kazi hicho.👇

































































No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇