Na Yahya Nsangi, Togo
Ukifika Seoul utajionea wadada wengi wasiotaka kujipodoa ili wavutie. Sababu kubwa wanadai kuwa mwanamke anayejipodoa anakuwa tayari kajigeuza bidhaa ya kuvutia wengine, hasa wanaume. Wao hawataki kuwa bidhaa. Umpende alivyo. Uvutiwe naye alivyo na wewe avutiwe naye ulivyo. Ukienda na akili zako za Rombo ukaanza kumnunulis vipodozi utashangaa ukipiga simu unajibiwa "wewe ni mrombo tafuta warombo wenzio"!
Hebu tutizame historia ya make-up tuone inasemaje?
Make-up ni fani iliyoaanza takribani miaka 6000 iliyopita. Madhumuni makuu yalikuwa mawili: kujificha(camouflage) na kutaka utamaniwe (attraction & affection)
Katika kitabu cha Jeremiah wakristo wanakatazwa kujipodoa. Jeremiah anasema anayejipodoa au kujirembesha anakosa roho mtakatifu. Katika kitabu cha wafalme anaelezewa malkia Jezebel kama malkia wa uovu. Moja ya sababu kubwa ni kujipodoa kwake kulikoendana na ushawishi mkubwa kwa mumewe. Alikuwa akimwambia mumewe huyu nataka afe, utauawa tu. Alikuwa mlimbwende haswaa.
Kwa maana ya vitabu hivyo (sijavitunga mimi) mwanamke wa kikristo hatakiwi ajipodoe. Atakosa roho mtakatifu. Lakini ingia kanisani ujionee!
Je kwa waislamu?
Wanawake wa kiislamu wanaruhusiwa kutumia make-up lakini kwa masharti:
1. Isiwe nia ni kwenda nje ya nyumba zao kwa minajili ya kuvutia watu au mtu asiyekuwa mume. Kama Yuko na mumewe pia anatakiwa apime je atazimua hisia za wengine? Yaani umejikwatua haswaa , umetoka na musee lakini njia nzima unaacha wanaume hoi. Au mnaenda kutembelea marafiki. Japo uko na mumeo unawapa taabu kina Chicco Paris. Kila saa shemelaaa mashalaaaa! Haiswihi. Sio mimi ni Quran. Ukitoka nje na mumeo jikwatua kwa kadri. Subiri mrudi ujikwatue utakavyo akutizame kama kolo linatizama bango.
2. Hiyo makeup iwe temporary sio permanent. Kwa hiyo tattoo zisizofutika ni haramu kwa mwanamke wa kiislamu. Sasa mnaotoboa pua au sikio? Mtaziba? Ni "makeup" aliyokupa mungu ndio permanent.
3. Makeup isiwe imetengenezwa Kwa vitu vilivyoharamishwa. Mfano makeup au perfume yako iwe Ina alcohol. Unajipulizia perfume unaenda msikitini kumbe mhhhh! Au nywele bandia ziwe na chochote kitokanacho na kitimoto.
Ikiwa haya matatu yatakiukwa basi mwanamke wa kiislamu naye kazuiliwa kutumia make-up sawa tu Jeremiah alivyokataza wanawake wa kikristo.
Hitimisho: wanawake wa Korea wako sahihi.
Nikuombe mama gati Brightness Bhoke Machango uendelee kuwa natural. Endelea kupaka samli . Sitaki roho mtakatifu asepe. Sawa?
Yahya Msangi

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇