Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Komredi Daniel Chongolo anaanza kesho ziara ya siku tano katika Mkoa wa Katavi ambapo atafanya kazi ya kuimarisha uhai wa chama, kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi pamoja na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.
Komredi Chongolo anatarajiwa kuwasili leo ambapo atalakiwa na viongozi mbalimbali, wanachama wa chama hicho pamoja na wananchi kwa ujumla.


No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇