LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 2, 2023

ALIYEKUWA DC TEMEKE MOBHARE MATINYI ATEULIWA NA RAIS DK. SAMIA KUWA MKURUGENZI MPYA IDARA YA HABARI (MAELEZO) NA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI

Official CCM Blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam, Mobhare Matinyi, kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na pia Msemaji Mkuu wa Serikali.

Matinyi amechukua nafasi hiyo baada ya kubaki wazi tangu September 23, 2023, Rais Dk. Samia alipomteua aliyekuwa katika nafasi hiyo Gerson Msigwa, kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni na Michezo.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus, jana, Oktoba Mosi, 2023, imesema uteuzi huo unaanza mara moja.

Mobhare Matinyi

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages