Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan ameteuliwarasmi
kuwa Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Kituo cha Dunia cha Uhimilivu wa Mabadiliko
ya Tabianchi (Advisory Board of the Global Centre on Adaptation - GCA).
Taarifa ya uteuzihuo iliwasilishwa na Mhe. Ban Ki-moon, Mwenyekiti wa
Bodi ya GCA na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa alipokutana na Mhe. Rais
pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi
uliofanyika Nairobi, Kenya.
Heshima hii ni utambuzi wa uongozi mahiri wa Rais Samia katika jitihada
za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi Afrika na duniani kote ambapo
Tanzania ni kinara kwenyeutekelezaji wa miradi mbalimbali barani Afrika.
Wajumbe wengine wa Bodi hiyo ni Rais wa Jamhuri ya SenegalMhe. Macky
Sall, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Mhe. Moussa Faki Mahamat,Rais
wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)Mhe. Akinumwi Adesina na Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF)Mhe. Kristalina Georgieva.
GCA ni taasisi kubwa duni
ani inayosimamia masuala ya uhimilivu wa mabadiliko ya tabianchi, ambapo hadi sasa imeweza kufanikisha upatikanaji zaidi ya Dola za Marekani bilioni 50. Tanzania ni miongoni mwa nchi za kwanza zitakazonufaika na fedha hizo katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇