LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 15, 2023

WAKALA WA VIPIMO YACHANGIA ZAIDI YA SH. BIL, 24 PATO LA TAIFA




Na Richard Mwaikenda, Dodoma

 Wakala wa Vipimo (WMA) imechangia zaidi ya shilingi bilioni 24 katika pato la Taifa katika muda wa miaka mitano kuanzia mwaka 2018/19 hadi 2022/2023.


Mafanikio hayo yamebainishwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA, Stella Kahwa alipokuwa akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO jijini Dodoma Agosti 15, 2023, kuhusu utekelezaji wa majukumu ya WMA kwa mwaka 2022/2023 na vipaumbele vyao kwa mwaka 2023/2024.


Kahwa amesema kuwa mafanikio hayo yanadhihirisha manufaa ya kuanzishwa kwa WMA kwa lengo la kupunguza gharama za uendeshaji na kusaidia maeneo mengine ya huduma za kijamii ambayo yana umuhimu na uhitaji mkubwa.


Mchanganuo wa mchango huo kwa kila mwaka ni kama ufuatao: -


Mwaka Mchango (Bilioni)

2018/2019 4,044,160,480.68

2019/2020 5,328,909,792.12

2020/2021 6,414,274,906.93

2021/2022 4,183,490,575.20

2022/2023 4,398,245,387.96

Jumla 24,369,081,142.89


Wakala wa Vipimo (Weights and Measures Agency- WMA) ni Wakala ya Serikali ambayo ipo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara. Ilianzishwa tarehe 17.05.2002 kwa agizo la Serikali (GovernmentEstablishment Order) Na.194 kupitia Sheria ya uanzishwaji wa WakalazaSerikali sura 245.  Kabla ya kuanzishwa kwake majukumu yake yalikuwa yakitekelezwa chini ya idara iliyokuwa ndaniWizara ya Viwanda na Biashara. 


Lengo kuu la kuanzishwa Wakala wa Vipimo ni kuboresha huduma zilizokuwa zikitolewa na Idara hiyo ya Vipimo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara na kupunguza gharama za uendeshaji kutoka katika mfuko mkuu wa Serikali kuu.


Ili kufanikisha lengo hilo, Wakala wa Vipimo inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo Sura Na. 340. Majukumu yanayotekelezwa kupitia sheria hii ni uhakiki na ukaguzi wa Vipimo, kutoa ushauri wa kitaalam kwa waundaji wa vipimo hapa nchini, kuidhinisha miundo ya vipimo mbalimbali kabla ya kuingizwa hapa nchini, ukaguzi wa bidhaa zilizofungashwa ambazo zinazalishwa kwenye viwanda vyetu vilivyopo hapa nchini na zile zinazotoka nje ya nchi.


 Wakala wa Vipimo katika utekelezaji wa majukumu yake unasaidia katika kujenga uchumi wa kisasa, shirikishi na shindani, msingi  mkuu wa kufanikisha haya ni kuwa na viwanda vinavyotumia ipasavyo vilivyohakikiwa na kukidhi matakwa ya kimataifa (Traceability to International Standards)ambavyo huongeza tija, ufanisi na usahihi wa vipimovya bidhaa zinazozalishwa kwenye viwanda hivyo kuwa shindani katika soko la ndani na la nje matokeo yake ni kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi na pato la Taifa.


Wakala wa Vipimo katika utekelezaji wa majukumu yake imeendelea kutoa mchango katika kuchochea maendeleo ya sekta za kiuchumi na kijamii nchini, kuchochea uzalishaji wa bidhaa unaozingatia vipimo sahihi, kuendelea kuchangia katika mfuko mkuu wa Serikali.



2 Majukumu ya Wakala wa Vipimo

Wakala wa Vipimo zinatekeleza majukumu yafuatayo: -

2.1: Kuhakiki vipimo vyote vinavyotumika kwenye Sekta za Biashara, Afya, Usalama na Mazingira;


2.2: Kuilinda jamii kuepukana na madhara yatokanayo na matokeo ya upimaji usio sahihi katika “Biashara, Afya, Usalama na Mazingira”;


2.3: Kuhifadhi vipimo vyenye usahihi wa ngazi ya kati (secondary standards) na kuhakikisha usahihi wake unakubalika na kulingana na vile vya kitaifa (primary standards) na vya kimataifa vipimo hivi hutumiwa na Wakala kuhakiki usahihi wa vipimo vinavyotumiwa na wafanyabiashara.


2.4: Kusimamia matumizi sahihi ya vipimo kwa njia ya 

kufanya ukaguzi wa mara kwa mara (Scheduled and Surprised Inspections);

2.5: Kukagua na kuhakiki bidhaa zilizofungashwa (Prepacked Goods) toka nje ya nchi na zile zinazozalishwa hapa nchini;

2.6: Kuidhinisha aina mpya ya vipimo vinavyoagizwa toka nje ya nchi na vinavyoundwa hapa nchini (Pattern Approval);

2.7: Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusiana na vipimo kwa Serikali, Mashirika, Taasisi na wadau wengine;


2.8: Kutoa vibali vya ugezi na leseni za ufundi na uundaji wa vipimo mbalimbali.

2.9: Kuiwasilisha nchi Ki-kanda na Ki-Mataifa katika masuala ya vipimo (EAC, SADCMEL na OIML).



3 Mchango wa Wakala wa Vipimo katika sekta za kiuchumi na kijamii

3.1 Kilimo.













No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages