LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 15, 2023

TOSCI YAFANIKISHA KUUZA DUNIANI MBEGU BORA ZA TANZANIA

 


 
Na Richard Mwaikenda, Dodoma

TAASISI ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), imefanikiwa kupata  Ithibati ya kimataifa ya ISTA Mei, 2018, ili kuiwezesha Tanzania kupata uwekezaji katika biashara ya mbegu kwa kuuza mbegu nchi yoyote duniani.


Hilo limebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Patrick Ngwediagi wakati wa mkutano na vyombo vya habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO jijini Dodoma Agosti 15, 2023, alipoelezea  kuhusu utekelezaji wa majukumu kwa mwaka 2022/2023 na vipaumbele vyao kwa mwaka 2023/2024.


Aidha, ametaja mafanikio mengine kuwa ni;

Kujiunga na Uanachama wa Skimu za Mbegu za Shirika la Kimataifa la (OECD) tangu Desemba 2016 faida yake ni kuiwezesha nchi kupata uwekezaji katika biashara ya mbegu kwa kuuza mbegu nchi yoyote duniani.


 Kupata uanachama wa Taasisi ya Kimataifa katika mbengu (UPOV) kuanzia Novemba 2015, uanachama huu umesaidia kuongeza wawekezaji wa ndani na nje katika ugunduzi wa aina mpya na bora za mbegu zinazofaa kulimwa na kutumiwa hapa nchini.

 Ongezeko la mbegu zilizothibitishwa ubora kitaifa na kimataifa kwenye mazao ya mahindi, mpunga, mtama, alizeti, mbegu za maboga, maharage, pamba, choroko, mbaazi, karanga, ufuta, ngano, kunde, njugu mawe, ulezi, tumbaku na maharage ya soya.


 Ongezeko la matumizi ya lebo za ubora: Matumizi ya lebo za ubora za TOSCI kumesababisha kupunguza tatizo la uwepo wa mbegu feki au zilizo na ubora hafifu.


 Kuanzisha au kuimarisha Ofsi za Kanda za TOSCI ili kutoa huduma zake kwa wadau kwa karibu zaidi.


Kuanzisha na kutumia mfumo wa TOSCI Online Application Service (TOAS).


Kujenga Maktaba ya Rejea ya Kijenetiki (Genetic Reference

Library): Maktaba hii imejengwa katika Makao Makuu ya TOSCI-Morogoro, lengo ni kuwezesha tathmini ya aina za mbequ zinazotumiwa na wakulima na kubaini uhalisia wake.


TOSCI ina jukumu la kusimamia shughuli za uzalishaji wa mbegu na biashara ya mbegu ili kuwahakikishia wakulima na wadau wengine kuwa mbegu wanazouziwa zina lebo ya ubora ya TOSCI na ni mbegu sahihi kwa matumizi. 


TOSCI ina makao makuu yake mkoani Morogoro, ina ofisi tano (5) za Kanda ambazo husimamia masuala yote ya uthibiti na udhibiti wa ubora wa mbegu katika Kanda husika ambazo ni Kanda ya Kaskazini (Arusha), Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Njombe), Kanda ya Ziwa (Mwanza), Kanda ya Kusini (Mtwara), Kanda ya Magharibi (Tabora).



No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages