MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha Mji Mwl. Mwajuma Nyamka amewataka viongozi na wanachama wa chama hicho wilayani humo kuendelea kuimarisha umoja kama njia ya kuharakisha maendeleo na uimara wa chama hicho.
Akizungumza katika ziara ya kutembelea viongozi wa mashina katika kata ya Misugusugu, mwenyekiti huyo alisema mojawapo ya njia za kuimarisha chama ni kuwa karibu na wanachama katika shida na raha.
Alisema nguvu za chama cha Mapinduzi kupitia wanachama wake hivi sasa zielekezwe katika kuhakikisha chama hicho kinaendelea kushinda kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2024 na 2025.
“Mshikamano ni jambo la lazima kwa wana CCM ili kujizatiti katika kupigania kupatikana kwa ushindi huo,” alisema mwenyekiti huyo.
Mwenyekiti huyo aliwataka wana ccm na wananchi wote kuendelea kutembea kifua mbele kutokana na ukweli kuwa wananchi wana imai kubwa na CCM.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇