Dk Happines Ruta |
Mtaalam wa afya kutoka Hospitali ya Rufaa ya Tumbi, Dk Happines Ruta amewaasa wanaume kuacha kuogopa vipimo vya ugonjwa wa tezi dume akisema kwa sasa kuna teknolojia mpya ya kupima tatizo hilo ambayo haimlazimishi mgonjwa kuingizwa kifaa sehemu za haja kubwa kama ilivyokuwa awali.
Aidha amewaasa wananchi nchini kupima ugonjwa wa ini. Ni kwamba, kutokana na sababu mbalimbali kama vile matumizi ya pombe kupita kiasi, sumu kwenye damu au maambukizi; ini hupata shida na kuvimba na kushindwa kufanya kazi vizuri.
Kwa mujibu wa Dk Ruta, virusi vya homa ya ini B na C husambaa kupitia damu, shahawa au maji maji mengine ya mwili. Virusi hivi vina uwezo wa kusambaa na kuambukiza mtu mara 100 zaidi ya virusi vya ukimwi.
Baadhi ya njia za kusambaa virusi hivi vya homa ya ini ni pamoja na;
1) Kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Mama aliye na maambukizi humuambukiza mtoto wakati wa kujifungua, iwapo hamna juhudi za matibabu za kuzuia maambukizi kuna uwezekano hadi asilimia 90 kwa mama kumuambukiza mtoto.
2) Kufanya mapenzi na mtu mwenye maambukizi ya virusi vya homa ya ini.
3) Kuchangia vifaa vyenye ncha kali kama sindano hasa kwa watumiaji wa madawa ya kulevya au wachora tattoo, miswaki.
4) Kuongezewa damu ambayo ina maambukizi ya homa ya ini.
5) Kunyonyana Ndimi ‘Denda’ na mtu mwenye maambukizi ya virusi vya homa ya ini.
6) Kuchangia taulo na mtu mwenye ugonjwa huu.
7) Kubadilishana nguo na mtu mwenye huu ugonjwa au kukumbatiana wakati mkiwa mnavuja jasho.
Tafiti za kitaalamu zinaonesha kuwa virusi hivyo ni hatari kuliko hata vya ukimwi kwa sababu vinaweza kuishi nje ya mwili wa binadamu (yaani nje ya mfumo wa damu) kwa siku saba. Virusi vya ukimwi (VVU) havina uwezo wa kuishi nje ya mfumo wa damu hata kwa dakika moja.
Dk Ruta pia amezungumzia umuhimu wa jamii kuwa na kadi za CHF ambayo ni Tsh30,000 kwa watu sita akisema kwamba ina msaada mkubwa sana.
“Unapokuwa na bima ya afya inakuwa rahisi kupata huduma za afya hata pale unapokumbwa na ugonjwa ghafla ukiwa huna fedha mkononi. Niwaombe sana Watanzania wenzangu tuchanganikie bima hii ya afya ambayo inapatikana hapa Misugusugu,” alisema Dk Ruta.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇