Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya TIBA ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), Profesa Abel Makubi akielezea kuhusu utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo katika mkutano na vyombo vya habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari -MAELEZO jijini Dodoma Agosti 3, 2023.
Prof. Makubi amebainisha kuwa katika mipango yao ya utekelezaji wa Bajeti ya Fedha ya Mwaka 2023/24, Serikali imetenga jumla ya TZS 55.9 billion kwa MOI ili kuboresha huduma za Tiba na shughuli za uendeshaji ;
Ametaja mipango yao mikuu kuwa ni;
Kuongeza ubora wa huduma zote ndani ya MOI ili kukidhi matarajio ya Wananchi ndani ya nchi na kufikia viwango vya Kimataifa na kuvutia Utalii Tiba
Kuanzisha huduma mpya tatu za kibingwa kibobezi ambazo bado zinasababisha rufaa nje nchi (Tiba ya baadhi ya Kiharusi kupitia Angio-suite, Tiba ya baadhi ya vifafa kupitia upasuaji na upasuaji wa kiuno kwa njia ya matundu (Hip arthroscopy)
Ukarabati wa Miundombinu ya Hospitali
Ujenzi mpya miundombinu;
Ujenzi wa jengo jipya la wagonjwa wa nje (OPD) ambalo litakuwa na vyumba 30 vya kliniki vya kisasa tofauti na vyumba 7 vilivyopo sasa.
Ujenzi wa hospitali ya kisasa ya utengamao, mazoezi ya viungo na upasuaji wa mifupa (Rehabilitation and Spine centre) katika kiwanja cha MOI chenye ukubwa wa hekari 10 kilichopo Mbweni Mpiji Mbweni jijini Dar es salaam.
Kuhakikisha vifaa tiba vinapatikana muda wote ambapo zimetengwa TZS bil 2 kwa mwaka huu
Kupunguza gharama za upasuaji kwa kununua vifaa moja kwa moja kutoka viwandani
Kuendelea kuwapa mafunzo wataalamu wetu ili kuwaongezea ujuzi ambapo wataamu 10 wanapelekwa kwenye mafunzo kupitia mfuko wa mafunzo wa Mama Samia. Aidha kuendelea kujij
engea uwezo watumishi wa Hospitali zingine za Kanda na Mikoa ili kupunguza mrundikano wa wagonjwa MO na kutoa nafuu ya gharama kwa Wananchi.
Kutoa elimu kwa kushirikiana na mamlaka nyingine ili kupunguza ajali za barabarani na kukabiliana na majeruhi kwa haraka.
Kuimarisha uwajibikaji na usimamizi kwa viongozi na watumishi ndani ya taasisi
Kuendelea kushirikiana na MUHAS, MNH. JKCI na Taasisi zingine katika kutoa Mafunzo na Tafiti katika eneo la Tiba ya Mifupa na Ubongo
Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akifafanua jambo wakati wa kuhitimisha mkutano huo ambapo amewataka wananchi wanapoumwa wajenge tabia ya kwenda hospitali kupata vipimo na tiba badala ya kwenda kwa waganga wa kienyeji.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇