LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 3, 2023

KATIBU CCM WILAYA KIBAHA MJINI ANENA KUHUSU BANDARI

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kibaha Mjini,  ndugu Salum Suleiman amewataka Watanzania wasikubali kupotoshwa kuhusu mkataba wa uwekezaji bandarini kwa sababu utakuwa na manufaa mengi ta Taifa.

 

Akizungumza katika ziara ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya Kibaha Mjini, Mwl Mwajuma Nyamka katika Kata ya Misugusugu wilayani humo, katibu hiyo anasema mkataba huo ni wa CCM sio mtu mmoja.

 

Katibu Suleiman alifafanua kuwa suala hilo lipo katika ilani ya uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2020, ibara ya 59 na ukurasa wa 92 kuhusu uboreshaji wa bandari.

 

“Serikali imepewa msukumo na chama kinasimamia kuhakikisha utekelezaji unafanyika, kuweni na imani na Serikali yenu na chama chenu, kina malengo mema kwa nchi hii,” amesema Suleiman na kuongeza kuwa suala la uwekezaji katika bandari sio geni, kwani hata kabla ya hawa wawekezaji wanaozungumza sasa, bandari imekuwa na wawekezaji mbalimbali.





No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages