Na Jumaane Gude, Temeke.
MKUTANO Maalumu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Temeke, umepokea na kuridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya CCM Jimbo la Temeke baada ya kuwasilishwa na Mbunge wa jimbo hilo, Dorothy Kilave.
Akifungua mkutano huo, jana, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Temeke, Zena Mgaya, alisema baada ya kupata taarifa ya utekekelezaji wa Ilani hiyo ya Mwaka 2021/22, kutoka kwa mbunge huyo, Dorothy, ameipitia na kurizishwa nayo.
Alisema mambo mengi yaliowasilishwa katika Utekelezaji wa Ilani hiyo, yana mchango mkubwa kwa serikali na Chama.
Kwa Upande wa Mbunge Jimbo hilo, Dorothy Kilave, alisema wanawajibika kila mwaka kutoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani kupitia kazi zao walizofanya za kiserikali ilimradi Chama Cha Mapinduzi kiendelee kushika dola.
Dorothy alisema aliyoyatekeleza pia ameshirikiana na Madawini wa Kata zote za jimbo hilo pamoja na watendaji kuanzia ngazi za chini.
Alisema katika utekelezaji wake amefanikisha mageuzi katika uchumi na maendeleo katika jimbo hilo, ikiwemo kuzifikia Kaya Masikini za jimbo hilo.
Pia amewezesha makundi na vikundi kwa vijana na wanawake na walemavu kupata mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri.
Alisema kundi la wanawake kuna idadi ya vikundi 75 vimekoposhwa Sh. zaidi ya milioni 500, kwa upande wa vijana vikundi 29 vilikopeshwa zaidi ya Sh. milioni 700 sawa na asilimia 24.
Pia Dorothy alisema kwa upande wa walemavu vikundi 18 vilikopesheka zaidi ya Sh. milioni nne, ambapo jumla ya vikundi vilivyokopesheka ni 112,zaidi ya Sh. bilioni moja.
"Naomba muone namna Rais Mama Samia anavyotoa fedha kwa ajili ya Manispaa yetu, chini ya usimamizi wa Meya wetu fedha hizi zimetoka kwa wingi watu wameweza kupata.
Mbunge wa Jimbo la Temeke Dorothy Kilave akizungumza wakati akiwasilisha Taarifa yake ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Mkutano Maalum wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Temeke, jana.
Mbunge wa Jimbo la Temeke Dorothy Kilave akikabidhi Nakala ya taarifa yake ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke Zena Mgaya, baada ya kuwasilisha taarifa hiyo.
Baadhi ya Wajumbe wakiwa kwenye Mkutano huo.
Baadhi ya Wajumbe wakiwa kwenye Mkutano huo.Baadhi ya Wajumbe wakiwa kwenye Mkutano huo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇