LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 18, 2023

MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA WA KIISLAMU YATAMBULIWA NA SERIKALI ZANZIBAR, KESHO MAPUMZIKO.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi,  amesema Mwaka mpya wa Kiislamu utatambuliwa na Serikali na kuwa siku ya mapumziko.


Amems hayo, kufuatia Serikali kuridhia ombi la Waislamu kuhusu kuiadhimisha siku hiyo ya mwaka mpya wa Kiislam na kuwa ya mapumziko kwa madhumuni ya kuipa hadhi na kuiongezea hamasa.


Ameyasema hayo katika hafla ya Maadhimisho  ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kiislamu wa 1445 Hijriya, yaliyofanyika katika Msikiti wa Munawar Mfikiwa, Wilaya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba, leo, Julai 18, 2023.


"Kwa Mamlaka ya kikatiba chini ya kifungu 6 (1)(a)cha Sheria ya Masuala ya Rais wa Zanzibar, Namba:3 ya 2020, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi  ametangaza rasmi kuwa kesho Jumatano itakuwa siku ya mapumziko Kitaifa Zanzibar", imesema taarifa ya Ikulu Zanzibar.


Katika haflahuyo, Rais  Alhajj Dk. Mwinyi ametoa mwito kwa Wazazi na Walezi kutimiza wajibu wa malezi ya vijana kuwa na kizazi  chema  chenye kumjua Mwenyezi Mungu kwa  kutekeleza maarimsho  yake na kujiepusha na makatazo  katika misingi  bora ya maadili kwa mujibu silka na tamaduni za dini. 


Pia amehimiza kuwa kila mwananchi anao wajibu wa kuhakikisha ni raia mwema na mzalendo wa kuijenga nchi kwa kuendelea kudumisha amani na utulivu uliopo..

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi, akihutibia katika Maadhimisho  ya mwaka mpya wa Kiislamu wa 1445 Hijriya, yaliyofanyika Msikiti wa Munawar Mfikiwa, Wilaya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba, leo, Julai 18, 2023

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages