Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamoud Jumaa amekanusha vikali suala la madai yanayoenezwa na baadhi ya watu kwamba Bandari ya Dar es Salaam, imeuzwa.
Akizumza jijini Dar es Salaam, amesema, madai hayo ni uongo na uzushisiyo na kwamba Bandari hiyo haiuzwi, bali ukweli ni kwamba mchakato unafanyika ni wa kuingia ubia na muwekezaji mwenye uwezo zaidi ili kiwango cha utoaji huduma kiwe bora na kuleta mapato makubwa zaidi kwa taifa.
Hamoud amesema, wanaodai bandari inauzwa ni propaganda zenye lengo la kuigombanisha serikali na wananchi, zinazozushwa na wale ambao wamekuwa wakipata maslahi binafsi kupitia bandari hiyo huku serikali ikiwa haipati mapato yanayolingana na umuhimu wa hiyo bandari.
Sanjari na M-NEC huyo, Mwanasheria Leonard Manyama ambaye pia Diwani wa Kata ya Wazo, ametoa ufafanuzi wa kina wa kisheria kuhusu mkataba mama juu ya uhalisia wa suala hilo, akisema, kulingana na mkataba mama, kisheria siyo usio na kikomo, wala wa miaka 100 kama inavyodaiwa.
Blog ya Taifa ya CCM (Official CCM Blog) tumeweza kurekodi alichosema M-NEC Hamoud na Mwanasheria. Tafadhali sikiliza vizuri video hapo👇
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇