Mawaziri watatu wametinga kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo kwenye Uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa Juni Mosi, 2023, kuitikia agizo la kwenda mkoani humo kuzitafutia ufumbuzi kero mbalimbali alizozibaini wakati wa ziara yake ya siku 7 mkoani humo.
Mawaziri waliotii wito huo ni Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, Naibu Waziri wa TAMISEMI, Deogratius Ndejembi na Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde.
Wananchi wakishangilia wakati Katibu Mkuu, Chongolo akihutubia kwenye mkutano huo wa hadhara."Ofisi ya Rais imetafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa xray na mochwari ifikapo julai mwaka huu. Pia Rais Samia anatafuta fedha kuwezesha afya ya watanzania zinaimarika, tutahakikisha tunakamilisha ujenzi wa zahanati ambazo bado hazijakamilika ili.wananchi waanze kupata huduma."
".Mkoa wa Iringa ni kati ya mikoa inayolima parachichi ,kilolo pekee imezalisha miche kwa ajili ya wakulima pia Nyololo tunajenga ghala kubwa ambalo litakusanya parachichi ya mkoa wote na kupelekwa nje ya nchi ambako kuna soko.".
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso,
"Nimeingia Mkoa wa Iringa ndani ya siku mbili kama maelekezo yako uliyoniitia nitayatembelea na kuangalia changamoto zilizopo na kuzitatua ili wananchi waanze kupata maji safi na salama."
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇