Haya yamesemwa na Afisa Mkuu Wateja Wakubwa na Serikali wa NMB – Bw. Alfred Shao wakati akiwasilisha mada katika Mkutano wa 37 wa ALAT uliofanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa AICC- Arusha ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdory Mpango alikuwa Mgeni rasmi.
Mkutano huu wenye Kauli Mbiu “Miundombinu iliyoboreshwa ni chachu ya tuoaji wa huduma bora katika Mamlaka za Serikali za Mitaa” uliwakutanisha zaidi ya watumishi 500 kutoka Halmashauri zote 184 za Majiji, Manispaa, Wilaya na Miji kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
Aidha, Bw. Shao alielezea kuwa, Benki ya NMB kama mdau wa maendeleo kupitia Halmashauri zote chini, imekuwa mshirika mkubwa sana kuboresha miundombinu ya elimu, afya, usafirishaji na mazingira na inaendelea kushiriki kikamilifu katika kutoa dhamana kwa Makandarasi zaidi ya 580 zenye thamani ya bilioni 49 katika hatua zote kuanzia hatua ya kuomba na kutekeleza miundombinu chini ya TARURA. Kupitia mifumo na mtandao mpana wa NMB umesaidia Serikali katika makusanyo ya mapato ya zaidi ya shilingi Trilioni 9.8 kuanzia mwaka 2018.
Lakini pia, kwenye utunzaji wa mazingira wamezindua kampeni ya upandaji miti milioni moja nchi nzima, ambapo hadi sasa wamepanda miti zaidi ya 550,000 pamoja na hiyo NMB imetenga kiasi cha shilingi Milioni 472 kama zawadi katika kampeni ya Tunza Mti Tukutuze kwa shule za Halmashauri zote Bara na Visiwani kushirikiana na Wizara ya TAMISEMI
Akisisitiza umuhimu wa kuyatunza mazingira kwa ajili ya maendeleo endelevu, Dkt. Mpango alizihamasisha Halmashauri kushiriki kikamilifu na kuwataka kufanya kama NMB walivyofanya kwenye kampeni ya kupanda miti milioni moja ambapo kwa kushirikiana na TAMISEMI wameandaa shindano la shule la upandaji miti lenye zawadi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇