Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Daniel Chongolo amewataka wananchi wa Mkoa Iringa kuhakikisha wanautumia vizuri Uwanja wa Ndege wa Nduli uliopo Iringa utakapokamilika kuongeza uchumi wao kwa kusafirisha mazao.
Aidha Chongolo amesema maamuzi wa Serikali kujenga upya uwanja wa ndege wa Nduli Mkoani Iringa ni kufungua fursa kwa wananchi wa kusini kuweza kusafirisha bidhaa za mazao ili kutafuta soko ndani na nje ya nchi.
Katibu Mkuu wa CCM amesema hayo Juni Mosi ,2023 muda mfupi baada ya kukagua upanuzi wa ujenzi wa Kiwanja cha Ndege Nduli, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku saba ya kukagua uhai wa chama na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.
Amesema Utalii utakwenda kufungua baada ya kukamilika kwa uwanja huo wa Nduli ambapo wananchi watapata fedha za kigeni na hayo ndio maendeleo ambayo Serikalo ya CCM inayaleta kwa wananchi wake.
Katika hatua nyingine Chongolo amewataka wananchi wa Iringa kuendelea kutunza utamaduni wa mkoa huo ili wageni wanaoingia wajue utamaduni sambamba na kuwarithisha kizazi kijacho badala ya kuendelea kuiga mila za nchi nyingine
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇