LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 6, 2023

SERIKALI MKOANI KAGERA YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUWAONDOLEA KILIO WAKULIMA WA KAHAWA.

Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Toba Nguvila.


Na Lydia Lugakila,

Bukoba


"Hakika ninyi wakulima  ni mashahidi na mmeonja uzuri wa Rais Dokta Samia Suluhu Hassan,huku mkikumbuka shida nyingi mlizopitia, ikiwemo kunyonywa na kuwepo kwa tozo nyingi kwenu Wakulima, pamoja na mifumo ya kizamani iliyokuwa ikitumika sasa yote hayo yamekwisha pongezi kwa kiongozi wetu"


Hiyo ni kauli ya Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Toba Nguvila katika mkutano Mkuu wa kawaida wa Therathini na tatu, msimu wa Mwaka 2023/2024 uliofanyika mjini Bukoba.


Nguvila amesema kuwa, awali Rais Samia baada ya kuona mateso makubwa wanayopitia  Wakulima hao wa kahawa aliamua, kumuelekeza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Kilimo ambao walikaa kikao cha kwanza Wilayani Karagwe, kikao kingine Bukoba mjini ili kuona namna ya kuboresha utaratibu mpya na mzuri ambao una manufaa makubwa kwa Wakulima kwa kuuza Kahawa yao kwa mnada badala ya  mfumo wa zamani ambao ulikuwa na hasara nyingi.


"Kwenye hili Rais wetu anahitaji pongezi nyingi tozo nyingi ziliondolewa sasa Wakulima kwa sasa hamlipi tozo anayelipa ni mnunuzi kwa zile tozo tano tu" alisema katibu Tawala huyo.


Aidha Nguvila amesema kuwa haya ni mageuzi makubwa kwenye zao la Kahawa ambalo linaangalia sana manufaa ya wakulima sio manufaa ya watu wa katikati huku akieleza kuwa sasa kila mtu anatamani kulima Kahawa kutokana na Mazingira kuwa mazuri kwa Sasa.


Amewataka wakulima wa Kahawa kutumia msimu huu kwa Kahawa zote kununuliwa kwa njia halali sio magendo ikiwa ni pamoja na kuepuka kutumia mifumo ya zamani inayowaumiza.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha AMCOS Katanga Romward Bajumzi amesema msimamo huo wa Viongozi hao wa Serikali umeleta neema na mafanikio huku akimpongeza Rais Samia na Viongozi wengineo kwa usimamizi huo mzuri ambao umewafanya wananchi Mkoani Kagera kulidhika na hatua hiyo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages