LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 6, 2023

DK. MWINYI AANZA ZIARA YA KUKIIMARISHA CHAMA LEO, AHIMIZA UMOJA NA MSHIKAMANO.,

Zanzibar, leo
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK. Hussein Ali Mwinyi amesema baada ya uchaguzi kumalizika ni muhimu kwa Chama na Wanachama kujenga umoja, kwa kuondoa makundi yote na kushirikiana kwa pamoja.

Amesema, wale ambao wanaendelea kukiuka taratibu na kuchangia kuwepo kwa makundi wanapaswa kuitwa na kuchukuliwa hatua na Kamati za maadili ili kuhakikisha nidhamu na mshikamano ndani ya chama unatamalaki.

Dk. Mwinyi ameyasema hayo katika mkutano wa viongozi  wa CCM ngazi ya Shina , Majimbo, Wilaya na Mkoa uliofanyika katika ukumbi wa Picadilly, Kombeni, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi, mwanzono mwa ziara yake leo ya kukiimarisha chama na kutembelea miradi mbalimbali kukaguautekelezaji wa Ilani ya Chama.

Ziara hiyo ya kukagua utekekezaji wa Ilani ya CCM kwenye miradi na kukiimarisha Chama ni ya kwanza kwake tangu awe Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.

Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi  akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza   katika Mkutano wa Mabalozi na Halmashauri Kuu za CCM Majimbo ,Wilaya na  Mkoa wa Magharibi Kichama  katika ukumbi wa Piccadiliy Kombeni Wilaya Magharibi "B"leo.
 
Washiriki katika ngazi mbali mbali katika  Mkutano wa Mabalozi na Halmashauri Kuu za CCM Majimbo,Wilaya na  Mkoa wa Magharibi Kichama wakimsikiliza   Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi(hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumzanao  leo katika ukumbi wa Piccadiliy Kombeni Wilaya Magharibi "B" (Picha na Ikulu, Zanzibar)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages