LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 7, 2023

DK MWINYI AFANYA ZIARA, AWAASA WANACCM KUIMARISHA MSHIKAMANO

Na Dismas Lyassa

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Zanzibar), Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK. Hussein Ali Mwinyi amewaasa wanachama wa chama hicho kuimarisha mshikamo na kuachana na makundi.


Dk Mwinyi alisema kunapokuwa na chaguzi kama ule wa ndani ya chama uliokwisha mwaka jana, ni kawaida wagombea kuwa na makundi; huyu atamtaka yule na mwingine atamtaka huyu, lakini mara baada ya chaguzi kumalizika, makundi yote ni lazima yavunjwe ili kushirikiana kwa pamoja kuimarisha chama.

Kiongozi huyo ameonyesha kukerwa na wenye kuendekeza makundi, akaagiza wale wanaobainika kuendelea kukiuka taratibu na kuchangia kuwepo kwa makundi kuitwa na kuchukuliwa hatua na Kamati za maadili ili kuhakikisha nidhamu na mshikamano ndani ya chama unatamalaki.

Dk. Mwinyi ameyasema hayo katika ziara yake Mkoa wa Mjini Magharibi, yenye lengo la kukiimarisha chama na kutembelea miradi mbalimbali kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama akiambatana na viongozi mbalimbali wa Serikali na chama akiwamo Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho (Zanzibar) Mohammed Said Mohammed (Dimwa).

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages