Na Scolastica Msewa, Kibiti
MBUNGE
wa viti maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani
Mheshimiwa Subira Mgalu amekabidhi Wanawake wa wilaya ya Rufiji na
Kibiti vyerehani 35 kwa lengo la kuwainua kiuchumi
wana mama hao.
Akizungumza
mara baada ya kuwakabidhi vyerehani hivyo Mgalu alisema kuwa Wanawake
wengi wamekuwa tegemezi sana kutoka kwa wanaume zao hivyo vyerehani hivi
vinakwenda kuwa chachu ya ukuzaji uchumi wa wanawake hao na ndani ya
jumuiya ya UWT.
Walionufaika
na mgao wa Vyerehani hivyo ni wenyeviti wa kila kata na makatibu wa
kila kata wa Jumuiya ya UWT pia ofisi za wilaya zimepata vyerehani
vitatu ili nao waweze kusimama kiuchumi kwa kuanzisha miradi ya
ushonaji.
"Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa
akisisitiza juu ya wanawake kuweza kujisimamia katika masuala yetu ya
kiuchumi ndio maana nimewapatia mitaji hii ili muweze kukuza uchumi wenu
mmoja mmoja au kikundi"Alisema Subira Mgalu.
Aidha
amewakumbusha wanawake kuwa mstali wa mbele katika kukemea ukatili wa
kijinsia unaoendelea kwa watoto wetu kwani Taifa letu halikuwai kuwa na
mambo ya ajabu katika maadili ,hivyo kila mzazi asimamie maadili kwa
mtoto wake na watoto wa mwenzie.
Mbunge
huyo amewataka wanawake hao kuvitumia vyerehani hivyo ili viweze
kuwainua kiuchumi na kuondokana na tegemezi ya waume wao.
Naye
Mwajuma Said ambaye ni mkazi wa Rufiji amempongeza Mhe. Subira Mgalu
kwa jinsi ambavyo amekuwa mstali wa mbele katika kuwapambania wanawake
wa Mkoa wa Pwani.
Aidha
amemwakikishia kuwa uchumi wa wanawake unakwenda kupanda kutokana na
kupewa mashine hizo na sio lazima wote tuwe washinaji hata kuvikodisha
inawezekana.
Kwa Upande
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kibiti Tatu Mkumba amesema kuwa Mgalu ni
kiongozi mwenye maono ya mbali katika jumuiya hiyo.
Aidha
amewataka Wanawake wote ndani ya Mkoa wa Pwani kuendea kumuombea kwa
Mungu ili aweze kufanikiwa na kuzidi kutuletea neema zaidi.
Mbunge Viti maalumu mkoa wa Pwani Subira Mgalu (kulia) akimkabidhi Moja ya vyerehani 35 Mwenyekiti wa UWT Kibiti Tatu Mkumba kwaniaba ya Wanawake wa UWT Wilaya ya Kibiti na Rufiji katika hafla fupi iliyofanyika wilayani Kibiti mkoani Pwani. (Na Scolastica Msewa).
Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Pwani Subira Mgalu (wa nne kuanzia kulia) katika picha ya pamoja wakati wakiimba Wimbo wa CCM na Wanawake wa UWT Kibiti baada ya kukabidhi vyerehani 35 KWA Wanawake wa Wilaya ya Kibiti na Rufiji katika hafla iliyofanyika wilayani Kibiti mkoani Pwani (na Scolastica Msewa)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇