LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 10, 2023

DISMAS LYASSA APITISHWA NA KAMATI YA UTEKELEZAJI UVCCM KIBAHA MJINI KUWANOA VIJANA WILAYA


MWANDISHI wa Habari mkongwe na Mtaalam wa masuala ya Uongozi na Utawala, ndugu Dismas Lyassa (kulia) amepitishwa rasmi na kamati ya utekelezaji Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya Kibaha Mjini kusaidia kuwanoa vijana wa wilaya hiyo.

Akizungumza katika kikao maalum, Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kibaha Mjini, Ramadhan Kazembe anasema wilaya imejipanga kuhakikisha vijana wananolewa vizuri katika nyanja mbalimbali.

Dismas Lyassa katikati mbele akiwa katika picha na pamoja na viongozi (Mwenyekiti wa UVCCM Kibaha Mjini Ramadhan Kazembe. Kushoto kwa Dismas ni  katibu wa UVCCM Kibaha Mjini).


UVCCM wilaya imekuja na mkakati wa kuanzisha kamati nne; kamati ya Habari, kamati ya fedha na uchumi, kamati ya maendeleo ya jamii na kamati ya hamasa, ambazo zitanolewa kisha zitashuka chini kwa maana ya kata na matawi kufanya jambo kama hilo pia, anasema Kazembe.


“Tumekuwa tukihitaji wanoaji, bahati nzuri tunaye ndugu yetu Dismas Lyassa, nakupongeza kwa kukubali ombi letu la kuwanoa vijana….tumekuja na kauli mbiu ya Vijana… Utumishi na ubunifu… tunatamani kuona mabadiliko makubwa katika umoja wa vijana,” anasisitiza Kazembe na kuongeza pia kamati imewateua wakufunzi wengine wawili kusaidia katika suala hilo.

Dismas Lyassa licha ya kusomea Uandishi wa habari na Mawasiliano ya Umma pia amesomea Uongozi na Utawala ngazi ya Stashahada ya Uzamili na amekuwa akifanya kazi kama mshauri, Meneja Miradi na pia kama Mhariri wa vyombo mbalimbali vya habari ndani na nje ya nchi.

Pichani chini Dismas Lyassa akijitolea kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya Mtaa wa Mkombozi, Kata ya Pangani ya Halmashauri ya Mji Kibaha.




No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages