LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 27, 2023

CHONGOLO: CCM ITAENDELEA KUUENZI NA KUULINDA MUUNGANO

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo, akisisitiza kuwa Watanzania wataendelea kuuenzi na kuulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa ajili ya manufaa ya sasa na ya baadae.


Chongolo amesema Muungano ni jambo kubwa la muhimu lililoasisiwa na Waasisi wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Aman Karume ambapo kwa pamoja waliunganisha fikra za Watanganyika na Wazanzibari na kuwa Watanzania.


Amesema hayo katika salam zake za kuwatakia Watanzania Sikukuu njema ya kumbukizi ya siku ya Muungano wa Tangayikana Zanzibar anbayo kilele chake kilifanyika jana.


Katika ujumbe wake huo Chongolo amesema CCM itaenzi na kuzidi kuhakikisha Muungano unaendelea kwa manufaa ya Watanzania wote hivyo kila mmoja atekeleze wajibu wake hasa katika kufanya kazi ili aone matokeo ya Muungano huo wenye historia ya kipekee Afrika.


“Ndugu zangu Watanzania nawaomba, kwa Umoja wetu, Wanaume kwa Wanawake, Vijana wa kike na wakiume tuzidi kujivunia na kuulinda Muungano wetu ili tuendelee kunufaika kama Taifa,” alisema Chongolo

Daniel Chongolo

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages