LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 4, 2023

UKOSEFU VIFAA TIBA KATIKA HOSPITALI ,VITUO VYA AFYA WAMKERA KATIBU MKUU CCM

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameeleza kwamba atafanya mazungumzo na Waziri wa Afya Ummy ili kuhakikisha Bohari ya Dawa (MSD) inapeleka vifaa tiba katika Vituo vya Afya na Hospital zote nchini ambavyo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 100.

Chongolo ameyasema hayo akiwa katika Kituo cha Afya cha Ilongero kilichopo Singida Vijijini wakati alipofika kwa ajili ya kukikagua na kuzungumza na watumishi pamoja na  wananchi katika eneo hilo ikiwa ni muendelezo wa ziara zake katika Mkoa huo kukagua utekelezaji wa Ilani na kusikiliza Changamoto zinazowakabili wananchi.

"Serikali imekwishatoa fedha kwa ajili ya ujenzi, ambapo baada kukamilika kwa ujenzi wa vituo vya afya na zahanati inabidi tija yake ianze kuonekana kwa Wananchi kwa kupata huduma za Afya. Hatuhitaji kuona majengo mazuri lakini hayana huduma.

"Hivi hii  hospitali ingekuwa imekamilika halafu hakuna huduma nani angefurahia, ingekuwa unatoka hapa unaenda umbali kutafuta huduma sawa au sio sawa?"

 Amefafanua Chongolo wakati akizungumzia umuhimu wa Wizara ya Afya inapeleka vifaa tiba kwenye hospitali na vituo vya afya ambavyo ujenzi umekamilika,lengo wananchi wapate huduma karibu na maeneo yao.




No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages