LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 4, 2023

OSHA YATAJA MAFANIKIO YAKE LUKUKI KITAIFA NA KIMATAIFA


Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Khadija Mwenda akizungumza kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Osha katika mkutano na vyombo vya habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO, jijini Dodoma Machi 4, 2023. Ametaja mafanikio lukuki waliyoyapata kitaifa na kimataifa.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari -MAELEZO, Zamaradi Kawawa akiongoza mkutano huo.


MAFANIKIO YA WAKALA KATIKA KUSIMAMIA SHERIA YA USALAMA NA AFYA NA HIVYO KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MIWILI YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA (6)


Katika kipindi hiki cha miaka miwili ya serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na Rais wetu Mpendwa, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Taasisi ya OSHA imepata mafanikio makubwa ambayo yametokana na uongozi wake madhubuti yanayoendana na utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala Ibara ya 130 (f) ambapo Chama kimewaahidi Watanzania kwamba kitajenga uwezo wa waajiri na wafanyakazi kuhusu afya na usalama mahali pa kazi.


Aidha, wote ni mashahidi na tunaona juhudi ambazo, Mhe.  Rais wetu, Amekuwa akizifanya kuhakikisha kuwa wawekezaji wanakuja kuwekeza nchini ikiwemo kuhimiza uboreshaji wa mazingira ya biashara na uwekezaji na hili ni pamoja na maelekezo mbalimbali katika hotuba zake na hata hivi karibuni tumeona katika mabadiliko aliyoyafanya kwenye miundo ya Wizara, suala la uwekezaji limepewa kipaumbele na kuhamishiwa katika Ofisi ya Rais.


Ndugu Wanahabari, OSHA ni taasisi wezeshi, hivyo ni jukumu letu kuhakikisha kuwa uwekezaji nchini unakuwa na tija na manufaa kwa wananchi pamoja na kulinda nguvukazi ya Taifa, ili kuwa na uzalishaji endelevu. Aidha, katika kusimamia hili, tumeweza kufanya maboresho yafuatayo;


Kupunguza Urasimu na kuboresha   Mifumo ya TEHEMA

       

Katika utendaji wa shughuli za wakala Mifumo ya TEHAMA imekuwa ni nyenzo muhimu katika kutoa huduma ambapo mifumo kama TANEPS, GePG, GAMIS, MUSE, E-office imesimikwa na inatumika.

 

Kubwa zaidi tumefanikiwa kusimika mfumo wa TEHEMA wa Usimamizi wa taarifa za kaguzi nchini (Workplace Inspection Management System (WIMS)) ambapo kupitia mfumo huu, huduma ya utoaji wa taarifa za ukaguzi, ajali na mafunzo unafanyika kwa njia ya kielektroniki na kwa kutumia mifumo hiyo tumeweza kufanikiwa kufanya yafuatayo:


Kupunguza muda wa kupata Cheti cha Usajili wa sehemu za kazi kutoka siku 14 hadi siku 1 kwa kuwa usajili unafanyika kwa njia ya kielektroniki na ambapo mteja ana uwezo kuprinti cheti chake cha usajili popote alipo (Online registration).

Kutoa Leseni ya Kukidhi Matakwa ya Sheria ya Usalama na Afya mahali pa kazi (Compliance License) kutoka siku 28 hadi siku 7 kwa sasa; na 


 Aidha, kupitia mfumo huu waajiri wanaweza kuingiza nyaraka zao zinazohitajika bila kufika katika ofisi za OSHA na kujifanyia tathmini ya namna walivyokidhi viwango vya usalama na afya (Self Assessment) hivyo kurahisha upatikanaji wa leseni na huduma zingine.


Kuondoa/ kupunguza Ada za Huduma mbali mbali

Kutokana na utafiti uliofanywa na Wakala kuhusu usajili wa sehemu za kazi pamoja na kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini. Ilibainika uwepo wa ada ambazo zilikuwa zinaongeza gharama za uendeshaji na kuchangia sehemu nyingi za kazi kutokidhi matakwa ya Sheria na kufifisha ushindani wao kibiashara. 

Hivyo, OSHA ilipendekeza ada hizo kupunguzwa ama kufutwa ambapo Mhe. Rais aliridhia ada hizo kufanyiwa marekebisho kupitia GN 719/2018, GN 999/2020, GN 496F/2021 na GN 478A/2022 kwa kuondoa na kupunguza jumla ya ada kumi na tatu (13) kama ifuatavyo: -

Kuondoa Ada ya Usajili wa eneo la kazi iliyokuwa ikitozwa kati ya Sh. 50,000 hadi Sh.1, 800,000;

Kuondoa Ada ya fomu ya usajili sehemu za kazi iliyokuwa ikitozwa Sh. 2,000;

Kufuta Faini zinazohusiana na ukosefu wa vifaa vya kuzimia moto ya Sh. 500,000;

Kuondoa Ada ya Leseni ya Ithibati iliyokuwa inatozwa Sh 200,000 kwa mwaka; 

Kuondoa ada ya Ushauri wa kitaalamu wa Usalama na Afya ya Sh 450,000.

Kufuta ada ya mafunzo ya elimu kwa umma iliyokuwa inatozwa kiasi cha Sh. 250,000 kwa kila mshiriki;

Kupunguza ada ya uchunguzi wa ajali iliyokuwa ikitozwa Sh. 500,000 mpaka Sh. 120,000. 

Kuondoa ada ya Kipimo cha Mzio (Allergy test) iliyokuwa ikitozwa Sh. 25,000 kwa Mfanyakazi

Kuondoa ada ya Kipimo cha Kilele cha Upumuaji (Peek Expiratory Flow test) iliyokuwa ikitozwa Sh. 10,000 kwa Mfanyakazi

Kupunguza ada ya huduma za ukaguzi wa mifumo ya umeme katika Vituo vya Mafuta vilivyopo vijijini kutoka Sh. 650,000 hadi Sh. 150,000. Punguzo hili lililenga kuhamasisha uwekezaji katika maeneo hayo, hivyo kupunguza athari zinazoweza kutokea kutokana na utunzaji wa mafuta kwenye chupa za maji na madumu, suala ambalo linahatarisha maisha ya wananchi katika maeneo hayo.


Ada zilizofutwa ama kupunguzwa na OSHA zinatarajiwa kuleta unafuu kwa Wafanyabiashara na Wawekezaji Nchini kwa kuwapunguzia gharama za uendeshaji. Kiasi kilicho futwa ama kupunguzwa kinakadiriwa kuwa zaidi ya Shiling Bilioni 35.

Lakini imempendeza Mhe. Rais fedha hizi zitumike katika kuimarisha mifumo ya kulinda wafanyakazi, ili waweze kuzalisha kwa tija



Kushiriki katika kufanikisha miradi ya kimkakati.

 Ndugu wana Habari, 

Taasisi yetu inashiriki kikamilifu katika Miradi ya Kimkakati inayotekelezwa na Serikali, kama vile Mradi wa kufua Umeme wa Bwawa la Mwl. Nyerere, Reli ya Kisasa (SGR), Bomba la Mafuta Ghafi linalotoka Hoima-Uganda hadi Tanga, Upanuzi wa Bandari zetu n.k. OSHA imekuwa ikifanya kaguzi za Usalama na Afya katika miradi hiyo kwa wakati na kwa ustadi mkubwa na hivyo kuchangia miradi hiyo kukamilika kwa wakati na katika ubora stahiki bila kuathiri nguvukazi inayotumika katika utekelezaji wa miradi hiyo.


Kuiwezesha Tanzania kutambulika katika Nchi za SADC katika masuala ya Usalama na Afya mahali pa Kazi.

Ndugu Wanahabari, katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita OSHA imeiwezesha Tanzania kupata Dawati la Usalama na Afya mahali pa Kazi katika Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).  Nafasi hii ni fursa kwa Nchi yetu kuweza kuuza na kubadilishana Utaalamu wa Mifumo ya Uendeshaji wa Taasisi za Usalama na Afya Kimataifa.  

Mwakilishi wa Tanzania kutoka OSHA alishindanishwa na wataalamu 48 kutoka katika Nchi 16 za Jumuiya na hatimaye Mwakilishi huyo wa Tanzania, alifanikiwa kuchukua nafasi hiyo. Pamoja na vigezo vingine vilivyotumika kupata mshindi, kigezo kimojawapo kilikuwa ni sifa ya Tanzania kuwa na mfumo madhubuti wa Usalama na Afya mahali pa kazi unaosimamia nguvu kazi na hatimaye kuwezesha kuwepo kwa ajira zenye staha.


Ndugu Wanahabari, hatua hii ni mafanikio makubwa kwa nchi yetu na OSHA kwa kutambulika Kimataifa kwa kuwa na wataalam wenye uwezo wa kusimamia mifumo ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi kwa kuzingatia vigezo vya Kimataifa. 


Kuchangia kuzalisha ajira nchini 


Katika kuhakikisha kuwa sehemu za kazi zinapata Leseni za Ithibati kwa wakati, OSHA imekuwa na utaratibu wa kufanya ukaguzi wa mifumo ya Usalama na Afya kisekta. Utaratibu huu umewezesha maeneo ya kazi kupata taswira ya hali halisi ya utendaji na vihatarishi vilivyomo kwenye maeneo yao na hatimaye kuchukua hatua mbalimbali za kuyarekebisha na kuyafanya yawe bora. Suala ambalo limepelekea kuzalishwa kwa ajira za wataalamu wa masuala ya usalama na afya kwa watanzania ndani na nje ya nchi.

 

Kuanzishwa kwa Programu Atamizi ya Wajasiriamali (SMEs Incubation Programme)


Kupitia program hiyo, Wakala umeweza kuifikia sekta isiyo rasmi hasa wakinamama wajasiriamali, wenye viwanda vidogo, vikundi vya wenye ulemavu, vijana pamoja na wachimbaji wadogo wa migodi nchini ambao ilikuwa vigumu kuwafikia kwa utaratibu wa kawaida wa ukaguzi wa maeneo ya kazi.


Programu hiyo yenye kauli mbiu “Afya yangu Mtaji Wangu” inajumuisha utoaji mafunzo bure kwa Wajasiriamali Wadogo ambapo katika kipindi hiki cha miaka miwili ya Awamu ya Sita jumla ya wajasiriamali 35,240 wamepewa mafunzo ya usalama na Afya mahali pa kazi, kupatiwa vifaa kinga. Aidha, tumeanzisha mfumo wa Kieletroniki unaowawezesha wajasiriamali kujisajili na kuwafikia katika maeneo yao ili kuwaelimisha pamoja na kushauri namna bora ya kuboresha mazingira yao ya kazi.


Kupitia program hii Wajasiriamali wadogo tunawatambua, tunawalea, na kuwapa elimu na kuwapa elimu ya kujikinga na athari za vihatarishi wanapokuwa katika shughuli zao za kiuchumi hivyo kuwawezesha kuwa rasmi. Aidha, tumeandaa mwongozo mahususi wa viwango vyao stahiki vya kukidhi matakwa ya Sheria ya Usalama na Afya ili waweze kuongeza ubora wa bidhaa zao na kukuza ushindani wa kibiashara katika soko ili nao waweze kuchangia mapato ya nchi kwa njia ya kulipa kodi.

Usalama na Afya Mahali pa Kazi kuwa Haki ya Msingi mahali pa kazi


Kama mtakumbuka vizuri, katika Hotuba ya Mei Mosi mwaka 2022 Jijini Dodoma, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, alitamka kuwa Nchi yetu ipo katika hatua mbali mbali za kuridhia Mkataba Na. 155 unaohusiana na masuala ya Usalama na Afya mahali pa kazi. 


Aidha, katika Mkutano wa 110 wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) uliofanyika Geneva, Uswisi Mwezi Juni, 2022, Nchi Wanachama waliazimia kwa pamoja kuridhia kujumuisha masuala ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi katika Miongozo ya ILO. 


Kutokana na azimio hilo, Mikataba Na. 155 na 187 inakuwa miongoni mwa Mikataba ya Msingi ya Shirika la Kazi Duniani (Core Conventions);

Mkataba Na. 155 wa Mwaka 1981 kuhusu Usalama na Afya Mahali pa Kazi (Occupational Safety and Health Convention) na 

Mkataba Na. 187 wa Mwaka 2006 wa Mfumo wa Kuhamasisha Masuala ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi (Promotional Framework for Occupational Health and Safety).


Hivyo, kufanya masuala ya Usalama na Afya mahala pa kazi kuwa si wajibu wa Kisheria pekee, bali kuwa Kanuni na Haki ya msingi mahali pa kazi (A safe and health working environment is fundamental principle and right at work). 


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages