LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 26, 2023

SERIKALI KUAJIRI WAHUDUMU WA AFYA 1,322 KUPAMBANA NA MARBURG KAGERA.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari Mkoani Kagera
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Zabron Yoti.
 

Na Lydia Lugakila, Kagera

Kufuatia uwepo wa ugonjwa Marburg Serikali imetoa mwelekeo  katika Mapambano dhidhi ya ugonjwa huo pamoja  na magonjwa mengine ya mlipuko katika kushirikiana kikamilifu na Jamii  huku ikitarajia kutoa ajira kwa watu 1,322 kutoka Vijiji, Vitongoji na mitaa yote ya Wilaya ya Bukoba na Bukoba mjini ili  kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kwa miezi 3.


Kauli hiyo imetolewa Machi 25, 2023 na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari Mkoani Kagera  juu mwenendo wa Ugonjwa wa Marburg.


Waziri Ummy amesema ili kuimalisha utekelezaji wa afua za Elimu ya Afya jumuishi hususani wakati huu wanapokabiliana  na ugonjwa wa Marburg na magonjwa mengine ya mlipuko ni wakati wa Kupambana bila kuchoka.


"Hivi sasa tunaanza na Halmashauri 2 ambazo ni Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na Bukoba Manispaa ambapo kila kitongoji tutakuwa na wahudumu 2 na kila Kijiji atakuwa ni mtu mmoja ambaye atasimama kama mratibu wa wale kwenye Vitongoji, na mtaa hususani Manispaa ambao watakuwa wahudumu watatu"alisema Waziri Ummy.


Aidha amesema kuwa tayari mafunzo hayo yanaendelea katika ukumbi wa Chemba na kwa wale waishio Kisiwa cha Goziba  Wilayani Muleba anakotokea mhisiwa wa kwanza   watachaguliwa na Serikali zao za mitaa na Vijiji na kwa upande wa kata ya Maruku Wilaya ya Bukoba watachukua zaidi Vijana angalau waliomaliza kidato Cha 4 ili wapambane kwa haraka.


Ameongeza kuwa baada ya kufanikiwa katika mradi huo kwa Mkoa wa Kagera zoezi hilo litafanyika kwa Nchi nzima 


Amesema hadi Sasa wameongeza wataalam 6 wa afya ikiwemo madaktari bingwa na bobezi wa magonjwa ya Figo huku akiwataka Wananchi kuondoa wasi wasi kwani hadi sasa hawajapatikana wagonjwa au wahisiwa wengine tofauti na wale wa Mwanzo.


Amewataka Wananchi kuendelee kuzingatia njia za kujikinga na tahadhali dhidi ya ugonjwa huo.


Waziri wa Afya amemshukuru mwakilishi mkazi wa shirika la Afya Duniani(WHO) Dkt. Zabron Yoti na Bi. Shalini Bahuguna, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la UNICEF kwa ushirikiano katika kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo wa Marburg.


Hata hivyo kwa upande wa Zabron Yoti amesema kuwa WHO utaendelea kuwa  karibu na Mkoa huo katika janga hilo huku akishukuru kuona shule hazijafungwa.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages