Na K-VIS BLOG/ Khalfam Said
Maandalizi ya mwisho ya Kikao Kazi cha 18 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini
(TAGCO) kinachoanza kesho Jumatatu Machi 27, 2023 jijini Dar es Salaam yamekamilika.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi katika kikao hicho kitakachofanyika kwa siku tano kuanzia Machi 27-31 katika Kituo
cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC).
Ili
kuhakikisha kila kitu kiko sawa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Selestine Kakele akifuatana na
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson
Msigwa pamoja na Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sarah Kibonde na Katibu Mkuu Bw. Abdul Njaidi wametembeela na kukagua ukumbi wa mkutano JNICC.
Kikao hicho kinawaleta pamoja Maafisa Habari na Maafisa Uhusiano kiasi cha 500 wote wa Serikali ili kujadili masuala mbalimbali yenye lengo la kuboresha utendaji kazi, kupeana mbinu mbalimbali za kufanya mawasiliano na namna ya kulinda taswira ya nchi na serikali, Katibu Mkuu wa TAGCO Bw. Abdul Njaidi amesema.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇