Mkuu wa wilaya ya Same, Kasilda Mgeni amewataka wananchi kuhakikisha wanatunza vyanzo vya maji kwa kuhakikisha wanapanda miti pembezoni mwa vyanzo vya maji
Amesema hayo kwenye kilele cha wiki ya Maji kitaifa akiwa anapanda mti na kuzitaka kila kaya kupanda mti kwenye maeneo ya nyumba zao,
Pia amesisitiza wananchi kuepuka kulima ndani ya mita 60 kutoka kwenye chanzo cha maji. Aidha amewaelekeza wataalamu wa maji kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi kuhusiana na suala zima la mita 60.
DC Kasilda Ameyasema hayo katika maadhimisho ya wiki ya maji wilaya ya Same yaliyofanyika katika kata ya Hedaru
Kaslida amewaomba Wananchi wote kumuunga mkono Mhe Rais Dokt Samiha Suluhu Hassani kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo katika jamii
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇