Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samwel Gwamaka ameunga mkono mbinu iliyotumiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mji wa Iringa (IRUWASA) ya kuunda vikundi vya ufugaji wa nyuki katika vyanzo vya maji ili wasaidie kuwang'ata watu wanaokwenda kuharibu vyanzo hivyo.
Ametoa tamko hilo wakati wa maswali kutoka kwa wanahabari katika mkutano wa NEMC na vyombo vya habari jijini Dodoma Machi 3, 2023, kuelezea utekelezaji wa majukumu ya baraza hilo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari -MAELEZO, Zamaradi Kawawa akisema neno wakati wa kuhitimisha mkutano huo.
Baadhi ya wanahabari wakiwa katika mkutano huo na wengine kuuliza maswali.Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Dkt Gwamaka akiunga mkono jambo hilo...
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇