Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew akihutubia alipokuwa akifunga mafunzo na mashindano ya Siku ya Kimataifa ya Wasichana na Tehema jijini Dodoma Machi 22, 2023. Wasichana kutoka mikoa 31 walihudhuria mafunzo na mashindano hayo na washindi kupatiwa zawadi za kompyuta mpakato. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).
Mhandisi Kundo amestaajabishwa na uwezo mkubwa wa wasichana walioweza kubuni APP mbalimbali za kitehama ikiwemo ya mahudhurio na lishe kwa watoto.
Kundo Mathew akiwakabidhi wasichana hao zawadi za kompyuta mpakato.
Wasichana waliobuni APP ya mahudhurio wakitambulishwa.
Naibu Waziri Kundo na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wasichana waliohudhuria mafunzo hayo.
Naibu Waziri Kundo (kushoto) akisindikizwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Justina Mashiba na Mwenyekiti wa Bodi ya UCSAF, Profesa John Nkoma.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇