VIONGOZI IRAMBA WAONGEZA WANACHAMA
Na HEMEDI MUNGA
KATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel
Chongolo amempongeza Mwenyekiti wa shina namba sita katika kata ya Ulemo, Evangelina
Samweli kwa kuongoza wanachama wa chama hicho na kazi kubwa ya kujenga chama
wanayoendelea nayo katika wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Chongolo amesema Mwenyekiti huyo na katibu wake wanaongoza
vizuri kwa kuongeza wanachama 38 kwa kipindi kifupi na kazi inaendelea.
Katibu Mkuu huyo, alitoa pongezi hizo leo wakati alipofanya
ziara ya kujenga uhai wa chama katika wilaya ya Iramba mkoani humo.
Halikadhalika, Chongolo alimuagiza mkuu wa wilaya
hiyo, Suleiman Mwenda kujibu baadhi ya kero zilizoibuka katika ziara hiyo.
Akijibu kero zilizoibuka katika ziara hiyo mbele ya
katibu mkuu huyo, Mkuu wa wilaya hiyo, Suleiman Mwenda aliwatoa hofu watu
wenyemahitaji maalumu kuwa serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ilikwishatoa
maagizo ya kujaliwa.
Mwenda alisema Halmashauri hiyo iliishatenga
takribani sh 4.3 milioni kwa lengo la kuhakikisha kundi hilo linakaa vikao vyao
kwa sababu ya kupanga mipango yao kwa mustakabali wa maisha yao.
Aidha, alifafanua kuwa serikali sikivu ya Dk. Samia
ilishatoa maelekezo, hivyo wanayafanyia kazi kwa umakini mkubwa.
‘’Ni lengo la serikali kuona watu wote wanapata haki
na huduma sawa, hivyo tunahakikisha kundi hili muhimu linapata mahijati
kulingana na utaratibu uliowekwa katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi,’’
alisema.
Aidha, aliongeza katika asilimia 10 za mikopo
itolewayo na serikali kundi hili la walemavu ni miongoni mwa wanufaika wa mkopo
huo.
‘’Ninashukuru
Mhe, Katibu Mkuu ninaomba nikuhakikishie kuwa walemavu tunawapa mikopo ya
asilimia mbili toka kwenye asilimia 10, na tayari vipo vikundi vya walemavu vimepatiwa
mikopo,’’alisema.
Pia, alisema kuhusu vikao wanavyotakiwa kukaa
walemavu Halmashauri imekwisha tenga takribani sh 4.3 milioni kwa mwaka wa
fedha 2022/2023, hivyo watakaa vikao vyao
Akizungumzia kuhusu chakula kwa lengo la
kuhakikisha ufaulu unaongezeka kwa shule zote, alisema wameweka utaraibu wa
kuhakisha chakula cha wanafunzi kinapatikana.
‘’Ni makubaliano ya vikao kuhakikisha watoto katika
shule za msingi na sekondari wanapata chakula kutokana na michango yetu,’’
alisema.
Hatua hiyo inatokana na
utafiti walioufanya na kugundua kuwa uwepo wa chakula shuleni unasabisha watoto
kuelewa na hatimaye wanafaulu katika masomo yao.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel
Chongolo akipata maelezo toka kwa Doktari Timothy Sumbe kulia, kushoto kwa katibu mkuu ni
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba na mwisho kushoto ni mkuu wa
wilaya hiyo, Suleiman Mwenda. (Picha na ofisi ya mkuu wa wilaya)
Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda akiwa katika mkutano pindi Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo alipotemelea wilaya hiyo leo. (Picha na ofisi ya mkuu wa wilaya)
Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman
Mwenda akiteta jambo na mmoja wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika
mkutano pindi Katibu Mkuu wa Chama hicho, Daniel Chongolo alipotemelea wilaya
hiyo leo. (Picha na ofisi ya mkuu wa wilaya)



No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇