LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 2, 2023

RAIS DK. MWINYI: ZANZIBARA INA MENGI YA KUJIFUNZA UZOEFU KUTOKA UFILIPINO

Ikulu, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar ina mengi ya kujifunza uzoefu na weledi kutoka nchi ya Ufilipino hasa kwenye sekta za mafuta na gasi, afya, utalii na uvuvi .

Pia Dk.Mwinyi amemuomba Balozi wa Ufilipino kuitangaza Zanzibar katika fursa mbalimbali ambazo zinapatikana visiwa humo.

Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo tarehe 02 Machi, 2023 Ikulu   Zanzibar  alipokutana  na Balozi wa  Ufilipino Tanzania  ,Marie Charlotte  G.Tang aliyefika kujitambulisha.

Naye, Balozi Marie Charlotte G.Tang amesema  ataongeza  uhusiano kati ya Ufilipino na Tanzania pia amekubali kuitangaza na kuwashawishi wawekezaji kutoka nchini mwake kuja Zanzibar kuangalia fursa za Uwekezaji zinazopatikana kutokana na kufanana mazingira kati ya  Ufilipino na Zanzibar .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe Dk. Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipokuwa katika mazungumzo  na Balozi wa Ufilipino Nchini Tanzania Mhe.Marie  Charlotte G.Tang,wakati alipofika Ikulu Jijini Zanzibar leo kujitambulisha.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages