Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisaini kitabu cha Wageni katika Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, ambako anafanya ziara ya kikazi kwa ajili ya majadiliano na Viongozi wa Taasisi za Kimataifa na baadhi ya viongozi waandamizi wa Serikali ya Uingereza kwa ajili ya Mipango ya maendeleo ya Tanzania.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Tanzania pamoja na maafisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza ambako anafanya ziara ya kikazi. Kushoto kwa Mhe. Waziri ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar Dkt. Juma Malik Akil, Mwambata Fedha, Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, Bi. Anath Lwenduru, na kulia kwake ni Balozi wa Tanzania- Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro, Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Japhet Justine.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, London,Uingereza)



No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇