Shirika la Ndege la Precision Air limedhamini upandaji miti 200 katika Shule ya Msingi Mtube, Kata ya Nkuhungu jijini Dodoma Machi 20, 2023 ikiwa ni moja ya shamrashamra ya kusherekea miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. Kampeni hiyo imeandaliwa na Taasisi ya Habari Conservation Organization.
Upandaji miti huo uliwashirikisha pia wanafunzi, walimu na baadhi ya wananchi wanaoizunguka shule hiyo.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Mtube wakihamasika wakati wa kampeni ya upandaji miti shuleni kwao.
Viongozi wa Taasisi ya habari Conservation Ordanization, Presicision Air, walimu na wanafunzi wa shule hiyo wakijiandaa kupanda miti.
Mratibu wa Precision Air Mkoa wa Dodoma, Gloria Kyara akipanda mti.
Wanafunzi wakielekezwa jinsi ya kuweka mbolea wakati wa upandaji miti.
Wanafunzi wakiwa na miti tayari kwenda kupanda.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Habari Conservation Organization, Bernard James akijiandaa kupanda mti.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mtube, Beneth Gikanka akipanda mti.
Mwalimu wa Mazingira wa shule hiyo akipanda mti.
Afisa Elimu Kata ya Nkuhundu, Salma Machaku akisaidiana na mwanafunzi kupanda mti.
Wanafunzi wakipanda miti.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Viongozi mbalimbali wakielezea umuhimy wa kupanda miti huku walimu na wanafunzi wa shule hiyo wakiahidi kuitunza miti hiyo....
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇