LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 8, 2023

OFISA UTUMISHI AOMBA USHIRIKIANO WA WATAALAMU NA MADIWANI

Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Julius Kimaro akizungumza na Madiwani na wataalum wa Halmashauri kwenye Kikao cha robo ya pili ya Mwaka.

 NA ODACE RWIMO NZEGA


OFISA Utumishi Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora Julius Kimaro amewaomba madiwani kushirikiana na watalaamu wa halmashauri hiyo ili kuweza kutekeleza miradi kwa weredi.
Kauli hiyo ameotia kufuatia kuwepo kwa kutokuelewana kwa baadhi ya hoja zikivutana kuhusiana na miradi inayotekelezwa katika baadhi ya Kata ambapo imeonekana kutokuwepo kwa ushirikiano wa karibu baina ya wataalamu na madiwani.
Alisema ili taswira ya halmashauri iwe nzuri na yakuvutia ni muhimu wataalamu wakishikamana na madiwani katika kutekeleza miradi inayoletwa na serikali ikiwa ni pamoja na ile inayotokana na nguvu za wananchi.
Alisema endapo madiwani wakiwathamini wataalamu katika kazi zao wanazozifanya kila siku katika maeneo yao italeta tija na manufaa makubwa kwa wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Nzega kwa ujumla.
“ Ndugu zangu najua ninyi ni wawakilishi wa wananchi katika jamii yetu na wataalamu ni wawakilishi wa serikali katika kutimiza majukumu yake ni vyema tukiwa kitu kimoja na kuondoa migongano aidha ya kimasrahi kwani hiyo itatuvunjia heshima na kuondowa uaminifu wetu kwenye jamii ”alisema Kimaro.

Hata hivyo ameshauri baraza la madiwani kutambua wajibu wao pindi wanapo tekeleza majukumu ya kulitumikia taifa huku akisisitiza uzalendo hasa katika miradi mikubwa iliyoletwa na rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmsahuri ya Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora Heneriko Kanoga alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha katika halmashauri hiyo.

Diwani wa Kata ya Mwantundu Paschal Lugonda ambaye alikuwa in mwenyekiti wa kamati ndogo ya kuchunguza mradi was kurejesha ardhi iliyoharibika unaotekelezwa kata ya Sigili akitoa taarifa ya kamati hiyo kwenye Baraza la madiwani

Alisema kwenye miradi mbalimali inayoendelea kutekelezwa na iliyokamilika ambayo inagharimu zaidi bilioni 1.9 ni fedha ya mama inayoenda kuwasaidia watanzania wote bila ya kubagua kabila lao,dini zao na vyama vyao.

“Hii ni ishara ya upendo wa rais wetu ukiangalia kuna baadhi ya maeneo hawakuwa na ndoto hata ya kupata maji safi,madarasa ya kisasa wala kupata zahanati na pengine hata barabara haikuwahi kufikiliwa kuwepo lakini Mama yetu Samia ameweza yote hayo”alisema kanoga.
Katika hatua nyingine Kanoga amevutiwa na utendaji wa Ofisa Utumishi wa Halmashauri hiyo kutokana na kuwa kuunganishi kikubwa cha madiwani na watumishi na kuwafanya kuwa kitu kimoja hasa pale wanapokuwa na majukumu yanalandana.
Alisema kumekuwepo na kutokuelewana kati ya wataalamu na madiwani hasa pale panapo jitokeza hoja ngumu lakini kwa sasa jambo hilo limeanza kutokomea na badara yake hukaa meza moja na kuangalia chanzo cha tatizo hilo limetokana na nini hasa.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages