LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 8, 2023

HALMASHAURI YA MJI WA NZEGA KUKUSANYA NA KUTIMIA BILIONI 23.27

Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Nzega Belbara Makono akizungumzia makisio ya bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024
ODACE RWIMO NZEGA.


KWA mwaka wa fedha 2023/2024 Halmasahauri ya Mji wa Nzega inatarajia kukusanya na kutumia zaidi ya bilioni 23 katika bajeti yake, fedha zitakazotokana na vyanzo mbalimbali vya mapato.

Akisoma mpango wa bajeti kwenye baraza la madiwani mkurugenzi mtendaji wa halmsahauri hiyo Shomary Mndolwa alisema fedha hizo zitatokana na vyanzo huru vya halmashauri,matumizi ya kawaida ( OC na PE) serikali kuu, Miradi ya Maendeleo,Miradi ya Wahisani,uchangiaji wa huduma za afya na mapato ya vijiji.

Alisema halmashauri inakisia kukusanya bilioni 2.74 kutoka vyanzo huru ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 3.68 kutoka kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 ongezeko hilo likitokana mwenendo mzuri wa makusanyo.

Alisema ili kuongeza mapato ya vyanzo vya ndani halmashauri imejiwekea mikakati mbalimbali ya kuhakikisha mapato yanakusanywa kwa ufanisi mkubwa huku akibainisha kuwa ni kupitia upya mifumo ya usimamizi na ufuatiliaji wa makusanyo ya mapato.

Mndolwa alisema wataendelea kuwashirikisha wadau mbalimbali katika kukusanya mapato ya halmashauri aidha mamlaka ya mapato Tanzania TRA na wadau wengine wa maendeleo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa mlipa kodi ili ajue uhimu wa kulipa kodi kwa hiari.

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Nzega Belbara Makono alisema bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 imeweka vipaumbele katika maeneo ya sekta ya Elimu,Afya,Usafi wa Mji,Utawala Bora,Kilimo na mifugo.

Alisema wataongeza mapato ya halmashauri kwa kuibua vyanzo vipya vya mapato ikiendana na kusimamia Usafi wa Mazingira sanjari na kuongeza asilimia za ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la nne kutoka asilimia 78 hadi kufikia 100.

Mkuu wa wilaya ya Nzega Mkoani Tabora Naitapwaki Tukai akizungumza na madiwani pamoja na wataalamu wa halmashauri ya Mji wa Nzega kwenye kikao cha baraza la madiwani.

Makono alisema wataongeza ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha pili kutoka asilimia 87 hadi kufikia 100 ikienda sambamba na kidato cha nne kutoka asilimia 80 hadi 100 kwa kufanya ufuatiliaji wa taaluma mashuleni.

Hata hivyo  Mkuu wa wilaya ya Nzega Naitapwaki Tukai aliwataka madiwani kushikama katika kuhakikisha miradi inayotekelezwa maeneo yao inakuwa na tija kwa jamii nzima ikiwa ni pamoja na kuitunza ili isihalibiwe na watu wasiokuwa wazalendo.

Alisema ni vyema suala la utunzaji wa mji likienda sambamba na utunzaji wa mazingira kwa kuhamasisha kila kaya kupanda miti mitano hii itasaidia kwa ustawi wa jamii kwa ujumla.

Alisema ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi na kuondokana na ukame kwa maeneo yetu ni mhimu utunzaji wa mazingira ukawa kipaumbele hasa kwa kupanda miti mingi kila sehemu kutokana na uhalibifu unaofanywa na baadhi ya watu kwa kukata miti na kuchoma mkaa.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages