LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 8, 2023

DIWANI AFURAHISHWA NA UONGOZI WA RAIS SAMIA

Diwani kata ya Mambali wilayani Nzega Mkoani Tabora Mkama Sadick akizungumzia mafanikio ya Kata hiyo chini ya serikali ya awamu ya sita.

 NA ODACE RWIMO NZEGA.


SERIKALI ya awamu ya sita imekuwa na mwendelezo wa miradi mikubwa na midogo hali inayoenda zaidi kwenye kuboresha maeneo yote muhimu yanayogusa watanzania wa hali zote.

Hiyo imeonekana hasa katika Nyanja za elimu,afya,maji umeme na miundombinu ya barabara huku barabara nyingi za vijijini zikipewa kipaumbele zaidi tofauti na ilivyokuwa hapo awali .

Diwani wa kata ya Mambali wilayani Nzega Mkoani Tabora Mkama Sadick alisema katika kata yake Rais Samia amemwaga fedha nyingi za maendeleo hasa katika Nyanja ya elimu afya maji na barabara ambapo ni kiasi ambacho hakuwa kukipata tangu uhuru wa nchi hii.

Akifafanua fedha ambazo mpaka hivi sasa zinatekekeleza miradi katika kata ya Mambali  kutekeleza ujenzi wa vyumba vya madarasa amepokea milioni 160 zilizojenga vyumba 8 vya madarasa katika shule zilizopo katani hapo.

Alisema hata upande wa Rais Samia Suluhu Hassan amewezesha kata hivyo kupata Zahati ambayo mpaka sasa imekamilika huku zaidi ya milioni 49 zikutumika katika ujenzi wa zahanati hiyo.

“ Unajua ukweli unatakiwa kusemwa na tutakuwa hatutendi haki kama tukikaa kimya kufuatia mazuri anayofanya mama yetu kwani sina hakika kama umemuacha mtu yoyote katika kugawana keki ya taifa mimi binafsi na wananchi wangu wa mambali tumefaidi sehemu kubwa ya keki hiyo”alisema Sadick

Alisema tumekuwa na shida ya mtandao wa barabara ambapo wakala wa barabara mjini na vijijini nchini TARURA amesaidia kufungua maeneo makubwa ambapo palikuwa hapapitiki lakini sasa tayari barabara zimetengenezwa.

Alisema kuna barabara ambayo imefungua uchumi wa wananchi wa kata ya Mambali zaidi ya km 13 ambayo ni Mambali –Itumbili,Itumbili –kikonoka huku zaidi ya km 18 zikiwa ni Mambali-uplya hadi Ugembe ambapo sasa panapitika kwa asilimia 100.

Hata hivyo baadhi wa wananchi wa kata ya Mambali wamempongeza diwani wa kata hiyo kwa mafanikio makubwa ambayo wanayapata kwenye  miradi ya maendeleo inayotekelezwa katani hapo.

Juma Hamis,Agnes Maganga na Matibya Masawe wakazi wa kata hiyo walisema maendeleo ya kata ya Mambali yamechagizwa na ushirikiano Wa diwani alionao kwa wananchi hata kwa viongozi mbalimbali huku wakitaja baadhi ya wahisani ambao pia wanasaidia kata hiyo.

Wanasema siyo jambo dogo hasa kupata miradi mikubwa kama walionao katani hapo kwa kipindi hiki hakika hawana namna ya kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan anavyo fanya kazi kazi ya kuiinua kata hiyo kwa kiasi kikubwa.

Hata hivyo walisema wanaunga mkono jitihadi zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita iwe mvua iwe jua wako na Rais Samia katika kuhakikisha wanashinda chaguzi za serikali za mita 2024 na uchaguzi Mkuu 2025 kwa kishindo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages