LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 9, 2023

NDEJEMBIi: HONGERENI PSSSF KWA KUTUMIA TEHAMA KUWAFIKIA WANACHAMA, AMEWAPONGEZA WAKATI WA MAADHIMISHO YA YA MIAKA 10 YA e-GA

Na Mwandishi Maalum, Arusha
Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Deogratius Ndejembi amezipongeza baadhi ya Taasisi za Umma, ukiwemo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kuwafikia wananchi kiurahisi kwa kutumia matumizi ya TEHAMA.

Mheshimiwa Ndejembi ametoa pongezi hizo jijini hapa katika hotuba yake ya ufunguzi sherehe za kutimiza miaka kumi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na kikao kazi cha tatu cha serikali mtandao, kinachokutanisha wataalam wa TEHAMA kutoka serikalini.

“Leo nimejionea kwenye mabanda pale PSSSF wameweza kuweka App ili kuweza kuona michango inavyokwenda Hivyo nielekeze e-GA kuendelea kufanya tafiti ili kuleta bunifu za mifumo ya TEHAMA itakayoliwezesha taifa kufanikiwa kuimarisha sekta za viwanda, biashara na uwekezaji kulipeleka mbele taifa letu kimaendeleo. Na katika hili nitoe pongezi pia kwa taasisi ambazo tayari zimeweza kuwafikia wananchi kiurahisi Zaidi na kuondoa urasimu wa makaratasi…” alisema Mhe. Ndejembi

Mheshimiwa Ndejembi amezishauri taasisi nyingine za umma kuitumia TEHAMA ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma za serikali kwa haraka.

PSSSF ina huduma za PSSSF Kiganjani na PSSSF Mtandaon. Huduma hizi ni suluhisho kwa wanachama, wastaafu na waajiri kuweza kupata huduma popote walipo na muda wowote kwa kutumia simu janja au kompyuta bila kuhitaji kufika kwenye ofisi za PSSSF.

Naibu Waziri katika ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Deogratius Ndejembi (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba, tuzo kwa ajili ya kufanikisha sherehe za miaka kumi ya e-GA na kikao kazi cha tatu cha serikali mtandao.  kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro, katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa e-GA, Mhandisi Benedict Ndomba.
Bi. Cleopatra Luse, Mtumishi wa Mfuko katika ofisi ya PSSSF Arusha, akitoa maelekezo kwa Mwanachama jinsi ya kujinga na huduma ya PSSSF kiganjani.
Bi. Cleopatra Luse, Mtumishi wa Mfuko katika ofisi ya PSSSF Arusha, akitoa maelekezo kwa Mwanachama jinsi ya kujinga na huduma ya PSSSF kiganjani.
Naibu Waziri katika ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Deogratius Ndejembi (wa nne kutoka kushoto) akipokea kitabu cha Mwongozo kwa Mwanachama kutoka kwa Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi (wa pili kushoto), wakati alipotembelea banda la PSSSF katika Maadhimisho ya miaka kumi ya e-GA, jijini Arusha. Wa tano kutoka kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa e-GA, Mhandisi Benedict Ndomba.
Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Peter Ulanga, atembelea banda la PSSSF katika kikao kazi cha 3 cha serikali mtandao, AICC Arusha.
 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages