LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 20, 2023

MJEMA: SERIKALI IMESHAFANYA MAKUBWA KUTEKELEZA ILANI, KAZI YA CCM ILIYOBAKI NI KUSIMAMIA YAKAMILIKE MACHACHE YALIYOSALIA

Na Bashir Nkoromo, Tanga
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema licha ya kwamba kazi kubwa imeshafanyika lakini bado ina kazi kubwa ya kuhakikisha ndani ya miaka miwili inakamilisha yote iliyowaahidi wananchi kupitia ilani yake ya Uchaguzi ya 2020-25.

Imesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, tayari imeshafanya makubwa mengi ambayo iliahidi katika Ilani hiyo, lakini bado kuna baadhi ya mambo machache ambayo inafanya kazi ya kuyasimamia kuhakikisha yanakamilika kwa kuwa ndiyo azma yake.

Hayo yamesemwa leo Jumapili, Februari 19, 2023 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Idara ya Itikadi na Uenezi Sophia Mjema, wakati akihutubia maelfu ya Wana CCM na Wananchi kwa jumla katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Tanga mjini

Amesma, mambo ambayo CCM inaweka nguvu kuhakikisha yanakamilika ni changamoto ambazo zimesalia katika huduma mbalimbali ikiwemo za  huduma za umeme, Afya, maji na elimu ambazo amesema CCM ina uhakika Serikali ya Awamu ya Sita itazishughulikia kwa kuwa tayari imeshazitambua changamoto hizo.

Mjema ambaye leo alikuwa katika siku ya pili ya ziara yake ya siku tatu mkoani Tanga, alitaja mifano ya hatua kubwa iliyokwishapigwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Samia ni kuboresha Sekta ya elimu ambapo katika nyanja hiyo miundombinu ya kufundishia na kusomea.

Amesema, kutokana na kuboreshwa mindombinu hiyo, sasa hakuna mtoto hata mmoja ambaye amekosa kusoma kwa sababu ya ukosefu wa vyumba vya madarasa kwa kuwa ujenzi wa nyumba vya madaraka umefanyika nchi nzima na pia kufuatia Serikali ya Rais Samia kutoa fedha nyingi kwa ajili ya elimu bila malipo watoto wengi wamepata fursa za kusoma bila kudaiwa ada.

Mjema amesema, upande wa afya, huduma zimeboreshwa ikiwemo kujengwa au kuboreshwa Hospitali, Zahanati na vituo vya Afya, nchi nzima, huku huduma ya mama na mtoto ikipewa kipaumbele. na kwa upande wa huduma za maji pia miundombinu imewekwa au kuboshwa kwa kiasi kikubwa mbali na changamoto zilizoslia katika maeneo machache.

 "Kwa kweli mambo mengi makubwa yameshafanyika, sasa jambo la muhimu ni kuhakikisha ninyi Wana CCM wenzangu na Wananchi kwa jumla tunamuunga mkono Rais Samia kwa yale ambayo ameshayafanya na yale ambayo anaendelea kuyafanya.

Na tunaposema tutakamiisha tuliyoahidi kuyafanya hatutanii, kwa sababu licha ya kuwa tunawapenda wananchi wetu, lakini pia bado ndiyo njia pekee ya kuhakikisha CCM inaenelea kushika dola maana ndicho chama ambacho bado ndiyo tegemeo la Watanzania", alisema Mjema.

Mapema, leo Mjema, alitembelea Kituo ha Afya cha Mama na Mtoto cha Lushoto mjini na kuona maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho ambao sasa umekamilika kwa takribani asilimia 95 na hivi karibuni kitaanza kutoa huduma.

Baadaye Mjema, alitembelea kiwanda cha kusindika majani ya Chai cha Mponde kilichopo Lushoto na kuona namna kiwanda kicho kilivyojizatititi kuhakikisha kinakuwa cha tija kwa wakulima wa zao hilo na pia kuchangia utoaji ajira hasa kwa vijana.

Katika ziara hiyo Mjema, amefuatana na Katibu wa NEC, Oganaizesheni Issa Ussi (Gavu) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Hamoud Abuu Jumaa na viongozi wengine mbalimbali.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Sophia Mjema akizungumza na maelfu ya Wanachama wa CCM na wananchi kwa jumla katika Mkutano wa hadhara uliofanyika leo Jumapili, Februari 19, 2023 mjini Tanga. Picha zaidi za ziara hiyo, Lushoto 👇
Katibu wa NEC Itkadi na Uenezi Sophia Mjema akisalimiana na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Lushoto  Godfrey Andrew alipowasili kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Huduma ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, leo.
Kushoto ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni Issa Ussi (Gavu).

Katibu wa NEC Itkadi na Uenezi Sophia Mjema akifurahia kina mama waliokuwa wakitumbukiza dufu wakimpokea alipowasili kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto, leo.

Wanachama wa CCM wakimlaki kwa shangwe Katibu wa NEC Itkadi na Uenezi Sophia Mjema alipowasili kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Huduma ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto mjini, leo.
Katibu wa NEC Itkadi na Uenezi Sophia Mjema akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Lushoto  Godfrey Andrew (kushoto), alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Huduma ya Mama na Mtoto katika Hospitai ya Wilaya ya Lushoto mkaoni Tanga, leo. pamoja naye ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni Issa Ussi (Gavu) na Mkuu wa mkoa wa Tanga Omary Mgumba.
Katibu wa NEC Itkadi na Uenezi Sophia Mjema akisaini kitabu cha Wageni baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Huduma ya Mama na Mtoto katika Hospitai ya Wilaya ya Lushoto mkaoni Tanga. Kushoto ni Mjumbe wa NEC Hamoud Abuu Jumaa na Katibu wa Oganaizesheni Issa Ussi (Gavu).
Jengo la Huduma ya Mama na Mtoto katika Hospitai ya Wilaya ya Lushoto mkaoni Tanga, ambalo Mjema alikagua maendeleo ya ujenzi wake.
Katibu wa NEC Itkadi na Uenezi Sophia Mjema akisoma kwa makini taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Huduma ya Mama na Mtoto katika Hospitai ya Wilaya ya Lushoto mkaoni Tanga.

Katibu wa NEC Itkadi na Uenezi Sophia Mjema akibadilishana mawazo na M-NEC Hamoud Jumaa (kushoto) na Katibu wa NEC Oganaizesheni Issa Ussi (Gavu). 

Kiwanda cha Majani ya Chai Mponde👇

Katibu wa NEC Itkadi na Uenezi Sophia Mjema akisalimiana na Wafanyakazi wa Kiwanda cha Majani ya Chai cha Mponde, alipofika kukagua kiwanda hicho.
Katibu wa NEC Itkadi na Uenezi Sophia Mjema (kushoto)  akimuuliza jambo Meneja wa Kiwanda cha Chai cha Mponde Saane Kwilaba (mweneye vazi jeupe) alipofika kukagua kiwanda hicho.
Katibu wa NEC Itkadi na Uenezi Sophia Mjema akitembelea Kiwanda hicho cha majani ya Chai cha Mponde. Kushoto ni Mjumbe wa NEC Hamoud Jumaa.
Katibu wa NEC Itkadi na Uenezi Sophia Mjema na ujumbe wake wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha Majani ya Chai cha Mponde Saane Kwilaba kuhusu sampuli mbalimbali za majani ya chai yaliyokwishasindikwa.
Katibu wa NEC Itkadi na Uenezi Sophia Mjema na ujumbe wake wakipata maelezo kutoka kwa MMsimamizi Mkuu wa Kiwanda cha Majani ya Chai cha Mponde ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PSSSF Injinia Temba Msemo. PSSSF na WCF ndiyo wasimamizi wa muda wa Kiwanda hicho kwa niaba ya Serikali.
Katibu wa NEC Itkadi na Uenezi Sophia Mjema na Ujumbe wake wakitoka kukagua kiwanda hicho cha majani ya chai.
mWananchi wa Mponde wakimshangilia Mjema, alipofika kuzungumza nao katika mkutano wa hadhara kwenye Kiwanda hicho cha majani ya Chai cha Mponde,
Mbunge wa Bumbuli Wilayani Lushoto Januari Makamba akizungumza na Wananchi wa Mponde baada ya kupewa nafasi na Mjema. Makamba pia ni Waziri wa Nishati.
Polisi akiimarisha ulinzi katika Mkutano huo wa Mponde, ikiwa ni utekelezaji wa agizo alilolitoa Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa wakati akiruhusu kufanyika mikutano ya vyama vya Siasa ambapo mikutano ya vyama vyote vya siasa itapewa ulinzi.
RC Mgumba akizungumza kwenye Mkutano huo wa Mponde.
Gavu akizungumza kwenye mkutano huo wa Mponde. Mkutano Tanga Mjini👇
"Tumeamua kuhamia CCM tumuunge mkono Mama yetu Rais Samia kwa kazi nzuri anayofanya. Tumeachana na Mbowe kwa sababu ni mroho wa madaraka... huyu hata akipewa Urais atataka awe rais wa milele", akisema Kiongozi wa Waliokuwa wanachama wa CHADEMA baada ya yeye na wenzake kutangaza kuhamia CCM katika Mkutano mkubwa wa Hadhara uliofanyika Tanga mjini. zaidi ya Wanachama hao 25 walihamia CCM.
Katibu wa NEC Itkadi na Uenezi Sophia Mjema akiwakaribisha wanachama wapya wa CCM waliohama kutoka Chadema kwenye mkutano huo wa Tanga Mjini
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Sophia Mjema akizungumza na maelfu ya Wanachama wa CCM na wananchi kwa jumla katika Mkutano wa hadhara uliofanyika leo Jumapili, Februari 19, 2023 mjini Tanga.

Wana CCM na Wananchi kwa jumla wakimsikiliza Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Sophia Mjema akizungumza nao katika Mkutano wa hadhara uliofanyika leo Jumapili, Februari 19, 2023 mjini Tanga.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages