LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 17, 2023

MBUNGE BYABATO AWAKUMBUKA MAAFISA USAFIRISHAJI KAGERA, AFANYA MAKUBWA.





Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Mhe, Stephen Byabato   ameungana na  Maafisa Usafirishaji (BODA BODA) wapatao 400 kutoka Manispaa   ya Bukoba ili kuona namna wanavyofanya kazi ikiwa ni pamoja na kutatua kero zinazowakabili wawapo katika Majukumu yao.


Mkutano wa Maafisa Usafirishaji umefanikiwa katika Uwanja wa Kaitaba Manispaa ya Bukoba.


Mhe, Byabato amekutana na waendesha Pikipiki hao ikiwa ni mara ya pili ambapo ametumia Kikao hicho kuwashauri kuhusu Mikopo yenye gharama na masharti nafuu ambapo Benki ya NMB imewapa ufadhili  na iko tayari kutoa Mikopo inayohitaji kiasi cha asilimia 20 ya thamani ya Chombo wanachotaka kuchukua.


"Mimi nikiwa mwakilishi wenu nimechangia kianzio cha Boda Boda 15 kwa kutoa asilimia 10 kwa kutoa Sh. Laki mbili na Elfu 70 ili nao wachangie Sh. Laki 2 na Elfu 70 ilete jumla ya Sh Milioni 2, laki 7 ili ziingie kwenye Akaunti"alisema Mhe, Byabato.


Byabato ameahidi kuendelea kuwaunga Mkono waendesha Pikipiki hao kwa kushirikiana na Taasisi mbali mbali ili kukopesha Pikipiki 200 zitakazosaidia watu kuondokana na uhalifu ambao umekuwa ukifanyika kutokana na ukosefu wa vipato.


Ameongeza kuwa ataendelea  kuwaunga Mkono ili Uchumi wa mtu Mmoja Mmoja Usonge mbele. 


Aidha amewataka Maafisa Usafirishaji hao kufuata Sheria pamoja kuwa waaminifu katika shughuli yao huku akimpongeza Rais Dkt Samia kwa namna anavyoendelea kuwajali katika miradi mbali mbali na kutoa fedha kwa wakati.


Kwa upandr wake Mkuu wa Wilaya ya Bukoba ambaye amekuwa Mgeni Rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo amesema kuwa kumekuwepo na  baadhi ya Boda boda wasio waaminifu ambao wanatumika katika uharifu kutokana na kushirikishwa na abiria wanaowabeba katika Vyombo vyao.


"Uwe unamjua Abiria uliybeba au Haumjui nakushauri mpeleke anakokwenda akikushirikisha kwenye uharifu usishirikiane naye kwani ikibainika ukakamatwa hadi kufikishwa Mahakamani, Wewe uliyeshirikiana na muhalifu kwenda kuiba utahukumiwa zaidi kuliko muhalifu huyo" alisema Kiongozi huyo.


Amewataka kuzingatia Sheria  wawapo Barabarani ili kuepuka ajali ambapo amedai  kuwa hakuna atakayevumiliwa endapo  Sheria.


Katika hatua nyingine amewasisitiza kuhakikisha wanafanya kazi kwa uadilifu na nidhamu ikiwa ni pamoja na kutumia vyema Pikipiki za mikopo kabla hawajazimiliki moja kwa moja.


Dc Erasto amewashauri  kujenga utamaduni wa kurejesha fedha za Mikopo ya Pikipiki kwa wakati ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kwani watakaofanya hivyo watampa kazi ngumu ya kuanza kuwafuatilia.


Haya hivyo Mkuu huyo Mkuu wa Wilaya hiyo, amesema kuwa tayari Rais Dkt Samia kamuamini na kumtuma akawahudumie wananchi wa Wilaya hiyo hivyo atamsaidia kwa nguvu zote kutokana na kuwa hakuja Kagera kuwa Mkuu wa Miti pekee.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages