LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 13, 2023

MADIWANI WILAYANI KYERWA WATAKIWA KUMALIZA KERO SUGU KATIKA MAENEO YAO.


Na, Lydia Lugakila Kyerwa.


Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa   Mkoani Kagera wameagizwa kuhakikisha wanatatua kero Sugu katika maeneo yao.


Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera Daniel Damian katika Kikao Baraza Baraza la Madiwani kilichofanyika  katika Ukumbi wa Halmashauri hiyo.


Daniel amesema kuwa Maagizo ya  Cha Cha Mapinduzi (CCM) yanaelekeza Madiwani kutimiza Majukumu yao katika kutatua kero Sugu  bila kujali itikadi za Chama za Vyama fulani.


"Chama chochote cha Siasa kuhakikisha kinatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambapo kila Diwani ahakikishe anashughulikia kero zote ili wananchi wasikwame katika shughuli zao ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwaamini" alisema Mwenyekiti huyo wa CCM.


Amesema Chama Cha Mapinduzi hakitamuomea huruma Diwani yeyote Mzembe katika eneo lake atakayeshindwa kuwajibika katika utatuzi wa Kero Sugu.


Katika Hatua nyinginezo Mwenyekiti huyo ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa  kutoa semina kwa Wakulima waishio Vijijini ili kuwasaidia kupata Hati Miliki  za Kimila zitakazomruhusu mtu yeyote kwenda popote hata kukopeshwa katika Taasisi za kifedha na kuendeleza shughuli za kilimo zenye tija.


Aidha ameitaka Ruwasa Wilayani humo kupeleka maji katika Taasisi zote za Kiserikali hasa katika Shule za Sekondari kwa wanafunzi wanaolala shuleni ili kuwanusuru.


Hata hivyo amempongeza Rais Dkt Samia namna alivyoipendelea Halmashauri hiyo katika Miradi mbali mbali ya Maendeleo.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilayani Kyerwa Daniel Damian akizungumza katika Kikao hicho.
Sehemu ya Madiwani hao wakifuatilia maelekezo ya Serikali

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages