LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 13, 2023

SERIKALI IKO TAYARI KUSHIRIKIANA NA TASNIA YA UTANGAZAJI KUWEKA MAZINGIRA BORA KISERA NA KIBIASHARA+video

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew akihutubia kwa niaba ya mgeni rasmi Waziri wa wizara hiyo, Nape Nnauye ambapo amewahakikishia wadau wa Tasnia ya Utangazaji kuwa Serikali iko tayari kushirikiana nao kuhakikisha inaweka mazingira bora ya kisera na kibiashara.

Aidha, Kundo amesema kuwa inabidi kwanza kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa muda mfupi wa uongozi wake amefanya mambo makubwa kuboresha sekta ya habari nchini.

Ameyasema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa Mwaka wa Watoa Huduma wa Sekta ya Utangazaji kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma Februari 13, 2023

Kundo akipongezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule kwa hotuba nzuri.

Akipongezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabiri Kuwe Bakari
Naibu Waziri Kundo akihutubia
Mhandisi Kisaka Andrew wa TCRA akiongoza mijadala.
Sehemu ya wadau wa tasnia ya utangazaji kutoka mikoa mbalimbali nchini wakiwa kwenye mkutano huo.





dau wa utangazaji akichangia hoja






PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Mhandisi Kundo akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano huo...



 

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages